TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, August 25, 2009

Pinda: Sijamtuma mtu kugombea ubunge

12:22 PM

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewaonya watu wanaotumia jina lake kutafuta nafasi za udiwani na ubunge wilayani hapa kuacha kufanya hivyo mara moja kwa sababu hajamtuma mtu yeyote kufanya hivyo.

Alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini Mpanda.

Alisema: “Kuna watu wanapitapita huku wanasema mimi nimewatuma waje kugombea huku Mpanda... wako wanaotaka udiwani na wengine ubunge, akiwaambia hivyo mshushueni kwa sababu mimi sijamtuma mtu yeyote. ”

Aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo ambao ulijumuisha viongozi wa chama hicho kutoka kata zote na majimbo matatu ya wilaya hiyo kuwa wabunge wa CCM wa Mkoa huo walikutana Sumbawanga wiki iliyopita ili kujipima na kutathmini kila mmoja anaendelea vipi.

Alisema CCM haipaswi kuruhusu watu waanze kampeni hivi sasa kwa sababu siyo sahihi na ni kinyume na kanuni za chama hicho.

“Chama kisiruhusu mtu ajitokeze sasa hivi na kuanza kampeni... tena aonekane anabebwa na chama. Chama katezeni, mwambieni asubiri wakati mwafaka ufike kwa mujibu wa kanuni za CCM, ” alisisitiza.

“Kama mtu anajipitisha kusalimia kwa wazee sawa, mwacheni afanye hivyo lakini siyo kuanza kampeni za wazi, mara unasikia katoa jezi, mara anashindanisha timu za kata au jimbo, hii ni kwa wote hata waliopo kwenye nyadhifa, kwani watu watajiuliza kwa nini unasubiri mwishoni mwa kipindi ndipo mtu aanze kuonekana na `powertiller', mara anatoa zawadi gani sijui?, " Alihoji Waziri Mkuu.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA