TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, August 26, 2009

Pinda akabidhiwa ripoti ya CAG ya ubadhirifu Kariakoo

3:59 PM

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amekabidhiwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyoiagiza kuhusu tuhuma za ukusanyaji ovyo na ubadhirifu wa mapato ya Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mkaguzi huyo, Ludovick Utoh, alikabidhi ripoti hiyo kwa Pinda jijini Dar es Salaam.

Ripoti hiyo inafuatia nyingine ya aina hiyo iliyotolewa na Utoh kuhusu Kituo cha Mabasi cha Ubungo aliyokabidhiwa Waziri Mkuu mjini Dodoma mwezi uliopita.

Akipokea ripoti kuhusu Soko la Kariakoo, Pinda alimpongeza CAG kwa kazi aliyoifanya na kuahidi kuwa kilichomo ndani yake kitafanyiwa kazi haraka.

Katika ripoti zote mbili, CAG aliainisha matatizo na kutoa mapendekezo ya kurekebisha hali ilivyo ili kuiboresha.

Waziri Mkuu alibaini, pamoja na mambo mengine, kuwa Kituo cha Mabasi cha Ubungo na Soko Kuu la Kariakoo ni maeneo mawili ambayo yangeingiza mapato makubwa kwa jiji, lakini ukusanyaji wake ni wa ovyo na kuna tuhuma za ubadhirifu.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA