TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, August 14, 2009

Mtaalam wa madini auawa nchini Kenya

12:03 PM

Mtaalam maarufu wa madini na vito vya thamani raia wa Scotland ameuawa nchini Kenya baada ya kuvamiwa na kundi la watu waliojizatiti kwa marungu, mikuki na mishale.

Mtaalam huyo Campbell Bridges, mwenye umri wa miaka 71, alishambuliwa na kundi la watu 20 katika kitalu anachomiliki cha hekari 600 karibu na mji wa kusini wa Voi.

Alijaribu kupambana na watu hao akishirikiana na mwanawe Bruce pamoja na wafanyakazi wake wanne raia wa Kenya lakini alikufa mara alipofikishwa hospitalini kutokana na majeraha aliyopata.

Polisi wanaendelea kuchunguza shambulio hilo ambalo linahusishwa na mzozo wa miaka mitatu wa kumiliki eneo hilo la machimbo lililokuwa linamilikiwa na Bwana Bridges.

Watu walioshuhudia wamesema mtaalam huyo alikufa kutokana na majeraha ya kushambuliwa kwa kisu. Hakuna mtu mwengine aliyekufa katika shambulio hilo lililotokea siku ya Jumanne.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA