TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, August 28, 2009

Mkuchika: TBC haijauzwa

12:23 PM
NA JOSEPH BURRA

SERIKALI imesema Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) haliwezi kuuzwa na kwamba, taarifa zilizoripotiwa ni uzushi na zimepikwa na kampuni binafsi zinazohofia ushindani.


Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, alipotoa tamko la serikali juu ya taarifa zilizoripotiwa na gazeti la MwanaHalisi, kuwa TBC imeuzwa kinyemela bila kuishirikisha Mamlaka ya Manunuzi (PPRA).


"Unaandikaje habari za uongo kupotosha umma kuwa TBC imeuzwa, hujamhoji hata Mkurugenzi wake …nilimwita Tido Mhando akasema hakuulizwa, wewe mwandishi gain? halafu tukiwafungia unaanza kupita balozi zote eti tunawaonea, zingatieni maadili yenu.


"Ushindani katika biashara usitufikishe mahali tukaanza kusema uongo, haiwezekani serikali inayotoa leseni iwe ya mwisho. Unayepewa leseni unataka kuwa wa kwanza ukishindwa unaanza kupotosha umma,” alisema Mkuchika.


Mkuchika alisema tuhuma hizo zinatokana na hatua ya TBC kuunda Kampuni mpya ya Star Media (Tanzania) Limited kwa ubia na mwekezaji aliyeteuliwa kihalali kutekeleza mabadiliko ya mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda dijitali.


Alisema TBC itaendelea kuwa shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na kwamba, Star Media (Tanzania) Limited ni kampuni tanzu ya TBC.


Waziri Mkuchika alisema uamuzi huo ulifikiwa kwa sababu kazi hiyo inayotakiwa ikamilike mwaka 2012 ni ya gharama na TBC peke yake isingeweza, kutokana na kuhitaji utaalamu wa kiufundi na fedha nyingi.


Alisema mchakato huo ulihusisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bodi ya Wakurugenzi wa TBC, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuchambua na kupendekeza mbia anayefaa.


Kwa mujibu wa Mkuchika, uteuzi wa mbia ulihusisha Bodi ya wakurugenzi wa TBC, wataalamu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.


Alisema TBC inachangia asilimia 35 inayotokana na majengo na minara yake na Kampuni ya Star Communication Network Technology ya China inachangia asilimia 65.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA