TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, August 28, 2009

Mabasi yatakiwa kufungwa mikanda kabla ya Oktoba

1:13 PM
Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Kombe alisema suala la kufunga mikanda katika mabasi sio jambo la hiari na halina mjadala ni wajibu wa kila mmiliki wa basi kuhakikisha anatekeleza agizo hilo kwani ni moja ya sheria za usalama barabarani nchini.
Alisema ifikapo Oktoba mosi basi ambalo litakuwa halijatekeleza agizo hilo litakamatwa na askari na kupelekwa mahakamani pamoja na kulizuia kuendelea kufanya kazi hiyo ya kusafirisha abiria.
Amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na mabasi ambayo hayatatekeleza agizo hilo na watapewa adhabu kali kwa kudharau agizo hilo.

Amesema lengo la agizo hilo ni kukabiliana na ajali za barabarani zimalizike ama zitoweke kabisa na kila basi linatakiwa liwe na cheses nzuri, na mikanda ya kuvaa abiria wanapokaa kwenye siti kwa kuwa abiria wamekuwa wakijeruhiwa na kufa kwa kukosekana kwa mikanda hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA