Mwanamziki wa R-N-B, Chris Brown jana amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita na adhabu na amepewa muda wa miaka mitano asije akafanya kosa lolote. Kifungo hicho kinafuatia kitendo cha
Chris Brwon kumpiga na kumwumiza mpenzi wake wa zamani ambaye pia ni mwanamziki, Rihanna.
Jaji Patricia Schnegg amemwambia Chris Brown kuwa akifanya kosa lolote, katika kipindi cha miaka mitano, atatupwa jela. Chris Brown atatumikia adhabu hiyo ya kazi ngumu akiwa uraiani kwenye jimbo lake la Virginia.
Bofya na soma ripoti jinsi Chris Brown alivyompiga Rihanna.
0 comments:
Post a Comment