TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, August 15, 2009

JK apokea hati za utambulisho za mabalozi

2:57 PM

Rais Jakaya Kikwete, amepokea hati za utambulisho za mabalozi wawili ambao wataziwakilisha nchi zao nchini.

Mabalozi hao ambao wamewasilisha hati zao za utambulisho katika shughuli fupi iliyofanyika jana Ikulu, jijini Dar es Salaam, ni balozi mpya wa Brazil, Francisco Carlos Soares Luz na balozi mpya wa Canada, Robert J Orr.

Akizungumza na Balozi Soares Luz baada ya kupokea hati zake, Rais Jakaya Kikwete alimwambia balozi huyo kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Brazil, na kuwa uhusiano huo umeimarika zaidi baada ya Tanzania kufungua ubalozi wake mjini Brasilia, mji mkuu wa Brazil.

Rais Kikwete pia amemwomba balozi huyo mpya kuangalia jinsi gani Brazil inavyoweza kubadilishana uzoefu na Tanzania katika eneo la maendeleo ya mifugo.

Aliongeza kuwa eneo jingine ni katika viwanda vinavyotegemea malighafi ya mazao ya kilimo ambako Brazil ina uwezo mkubwa.

Balozi Soares Luz alisema kuwa ataelekeza nguvu zake kuyashawishi makampuni ya Brazil kuja kuwekeza Tanzania.

Katika mazungumzo yake na Balozi Orr wa Canada, Rais Kikwete aliishukuru nchi hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika sekta mbali mbali za maendeleo.

Naye Balozi Orr alimsifu Rais Kikwete kwa jitihada zake katika kuleta amani katika eneo la Maziwa Makuu na kumhakikishia kuwa Canada itaendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo za Tanzania.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA