Wajumbe wakipiga kura
Aliekuwa Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,
Samuel Sitta akishukuru kwa furaha muda mfupi baada ya kutangazwa
mshindi wa nafasi hiyo kwa kura 469 dhidi ya mpinzani wake,Mh. Hashim
Rungwe katika uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita. Akitoa Neno la
Shukrani mara baada ya kupata nafasi hiyo,Mh. Sitta amewashurukuru
Wajumbe wote wa Bunge la Katiba kwa kuweza kumpa nafasi hiyo adhimu.Pia
amempongeza mpinzani wake, Mh. Hashim Rungwe kwa kukubali matokeo hayo.
Picha Juu ni Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo
Mwenyekiti
wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba mteule Mhe Samwel John Sitta akitoa
neno la shukurani kwa Wajumbe kwa imani waliyoonesha kwake kwa
kumchagua kwa kura nyingi kushika nafasi hiyo. Picha zote na Deusdedit
Moshi, Dodoma.

Katibu
wa Bunge Thomas Kashilila akiongea na waandishi wa habari(hawapo
pichani)kuhusu kukamilika kwa uteuzi wa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti
wa Bunge Maalum wa Katiba Ofisi Kwake Mjini Dodoma.Picha na Oweni-Bunge
0 comments:
Post a Comment