Meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama
cha Mapinduzi (CCM), Bw. Jerry Silaa akihutubia katika mkutano wa
kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila kata ya Mgama, jana.
Jerry
Silaa wa pili kutoka kushoto akiwa katika mkutano huo. Kushoto ni
mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM, Bw. Godfrey Mgimwa na
kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga,
Anthony Mavunde kutoka UVCCM Dodoma na Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa
Hassan Mtenga.
Mmoja wa wananchi akiserebuka huku akiwa amebeba beseni lake la ndizi katika mkutano huo.
Jerry
Silaa kushoto akishiriki kuimba nyimbo za kuhamasisha katika mkutano
huo wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila. Kulia ni
Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga na Anthony Mavunde
kutoka Dodoma wakijumuika pamoja.
Wananchi wakimlaki mgombea ubunge wa Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa wakati alipowasili katika kijiji cha Ibumila kata ya Mgama.
Jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi katika mkutano huo.
Wananchi wakimlaki Godfrey Mgimwa kwa kumbeba juu juu, wakati alipowasili katika kijiji cha Ibumila kata ya Mgama.
Kada wa CCM, Fredrick Mwakalebela akimpigia debe Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Ibumila kata ya Mgama wakati wa mkutano huo jana. 
Godfrey Mgimwa akivishwa mgorole na wazee wa kimila kama ishara ya heshima mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Ibumila kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana.
Meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama
chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa kulia akiteta jambo na Mgombea
ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey
Mgimwa wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye
kijiji cha ibumila kata ya Mgama halamashauri ya wilaya ya Iringa
vijijini mkoani Iringa, Jerry Silaa amewaomba wana Ibumila kumchagua
Godfrey Mgimwa ili kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiacha aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo Marehemu Dk. William Mgimwa.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA)
0 comments:
Post a Comment