TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, March 11, 2013

Watatu wafariki ajali ya basi Singida.

4:16 PM
Na Emmanuel Michael,
Singida


Watu watatu wamefariki na wengine 25 wamejeruhiwa baada ya ajlai ya basi la Green Star waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es salaam kwakielekea Kahama kugonga lori mkoani Singida.


Kwa mujibu wa mashuhuda basi hilo likiwa eneo la Isuna barabara kuu ya Dodoma – Singida saa 11 jioni wakati likijaribu kulipita lori lililokuwa limebeba mbao dereva alishindwa kulimudu ndipo akaligonga lori hilo kwa nyuma.


Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dokta Suleimani Mtani amesema kuwa majeruhi wengi wamevunjika miguu, mikono, migongo na kuumia vifua.


Polisi wamesema kuwa wanachunguza chanzo cha ajali hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA