TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, March 4, 2013

Wananchi wenye hasira waua dereva

11:21 PM
WATU wawili wamefariki dunia wilayani Ileje mkoani Mbeya, akiwemo dereva ambaye alishambuliwa na wananchi wenye hasira, baada ya kumgonga mtoto Lucy Kisunga (5) aliyekuwa akivuka barabara.

Tukio hilo, limetokea juzi jioni katika eneo la Ikumbilo, ambapo dereva Kawawa Mwakenga (37), aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Haice yenye namba za usajili T 108 AFL, alimgonga Lucy na kusababisha kifo chake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamule alisema dereva huyo baada ya kumgonga mtoto, alikimbilia kwenye duka lililopo jirani na eneo hilo na kuegesha gari lake ili kukwepa hasira za wananchi.

Alisema wananchi wenye hasira, walimfuata dereva huyo kwenye duka alikojificha na kuanza kumshambulia kwa mawe na virungu hadi kusababisha kifo chake.

Alisema chanzo cha ajali hiyo, bado kinaendelea kuchunguzwa na kutoa onyo kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.

Kwa upande wake, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Jim Mgode alisema chanzo cha ajali hiyo, ni mwendo kasi wa gari hilo kitendo ambacho kilisababisha derava ashindwe kulimudu.

Alisema madereva wengi, wanapofika eneo hilo wamekuwa na tabia ya kukimbiza magari kwa mwendo kasi bila kujali mbele yao kuna kitu gani.

Alisema dereva huyo, pia alishindwa kuchukua tahadhari, ikizingatiwa siku hiyo kulikuwa na gulio katika eneo hilo.

Chanzo:-mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA