
Meneja Mawasiliano na Kumbukumbu wa
Shirika Hodhi la Mali ya Mashirika ya Umma (CHC) Joseph Mapunda
(kushoto) akimpa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia)
leo ,jinsi Shirika hilo linavyofanya tathmini ya mashirika ya umma
yaliyobinafsishwa na utendaji wa mashirika hayo wakati alipotembelea
banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini
Dodoma

Mkuu
wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi
jinsi Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] inavyosaidia katika
kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa yakifanyika
kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi za
serikali na taasisi zake. Mkuu Mkoa huyo alipata maelezo hayo kutoka kwa
Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato
(kulia) alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya
wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.

Mchambuzi
wa Mifumo ya Komputya Mkuu Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti
ya TEKNOHAMA ya kifedha , Wizara ya Fedha Margethi Ambrosi Nembo
(kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone
(kulia) leo mjini Dodoma jinsi kuingiza mishahara na malimbikizo ya
watumishi wa umma kwa kutumia TEKNOHAMA . Mkuu Mkoa huyo alikuwa katika
maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Mkuu
wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto kwa
watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo
itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri
ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini.
Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipotembelea banda
la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini
Dodoma.
0 comments:
Post a Comment