
Rais Jakaya Kikwete akiweka mkasi mara
baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Karakana na ndege
za shirika la ndege la Precision Air jana kwenye uwanja wa ndege wa
Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es salaam kulia ni Bw Bw. Michael
Shirima

Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika la ndege la Precision Air
Bw. Michael Shirima katikati mara baada ya kuzindua Karakana ya ndege za
shirika hilo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la
Precision Air Bw. Alfonce Kioko

Rais Jakaya Kikwete akihutubia wageni waalikwa katika uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la ndege
la Precision Air Bw. Michael Shirima akimkabidhi zawadi Mh Rais Dk.
Jakaya Kikwete mara baada ya kuzinduz rasmi karakana na ndege za shirika
hili (Hanga) kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jana jijini
Dar es salaam, Karakana hiyo itakuwa na ikihudumia ndege za shirika hilo
la mashirika mengine pia lakini pia itapokea wanafunzi walio kwenye
mafunzo ya Uinjini wa ndege kutoka katika vuo vya ndani.

Mmoja wa mainjinia wa ndege za shirika hilo akirekebisha moja ya ndege za shirika hilo iliyoko kwenye (Hanga) Karakana hiyo.

Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Precision Air Bw. Alfonce
Kioko alipokuwa akitoa maelezo wakati wakati Rais alipokuwa akikagua
Hanga hiyo, kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mzee
Peter Kisumo mara baada ya uzinduzi huo kulia ni Mkurugenzi wa Hoteli
ya Kibo Palace ya Arusha.

Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.

Wafayakazi wa Precision Air wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.

Mkurugenzi wa Hoteli ya Kibo Palace ya Arusha Bw Vicent Laswai naye amehudhuria katika uzinduzi huo kama mdau wa Utalii.

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha
ya pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe pamoja na wakuu
mbalimbali wa shirika la ndege la Precision Air na wafanyakazi wa
shirika hilo mara baada ya uzinduzi wa (Hanga) hiyo
0 comments:
Post a Comment