TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, July 20, 2012

MJENGWABLOG INATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

11:26 AM
KWA mara nyingine, Watanzania  tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea jirani na kisiwa cha Chumbe, Unguja. Ndugu zetu wapatao 60 tayari wameripotiwa kupoteza uhai. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu.


Mjengwablog, kama chombo cha jamii cha habari na mawasiliano kinatoa salamu za rambirambi kwa  wahanga wote wa msiba huu mkubwa. Na  tunachukua fursa hii kumpa mkono wa pole  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa  Dr.  Jakaya Mrisho Kikwete, vivyo hivyo, mkono wetu wa pole umfikie Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar.

Mjengwablog inaungana na Watanzania wote katika siku hizi tatu za maombelezo kwa kutorusha habari na picha za matukio yenye kuashiria sherehe na burudani.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA