Afisa Muandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Tanzania Nd. Juma
Kimtu akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi Mchango wa Maafa wa Shilingi 10,000,000/- hapo ofisini kwake Mbweni
nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Nyuma yake ni Meneja Msuluhishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar {
ZSSF } Nd. Khamis Phil Phil Than.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea mchango
wa Maafa wa shilingi 10,000,000/- kutoka kwa Meneja Msuluhishi wa Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } Nd. Khamis Phil Phil Than hapo
katika Ofisi yake iliyopo Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya
Mji wa Zanzibar.
---
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewanasihi
Wananchi kuendelea kuiamini Serikali katika kupokea Taarifa zake hasa
wakati wa kutokea Majanga na Maafa.
Nasaha hizo amezito hapo katika Ofisini yake iliyopo Baraza la
Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akipokewa mkono
wa Pole kutoka kwa Taasisi mbali mbali za Umma na Kijamii.
Salamu hizo za mkono wa pole zimetolewa kwa Balozi Seif na Uongozi wa
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } na ule wa Hifadhi ya Taifa
ya Jamii ya Tanzania { NSSF } ambapo kila moja ilikabidhi mchango wa
Shilingi Milioni kumi { 1,000,000/- }.
Balozi Seif alisema Jamii kujenga tabia ya kuiamini Serikali hupelekea
kuwepuka kuchanganywa wakati wa kupokea Taarifa hizo kutoka vyombo
vya Habari vinavyopokea Baadhi ya Taarifa zisizo rasmi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa mifuko hiyo ya
Hifadhi ya Jamii Bara na Zanzibar kwa kufikiria jambo hilo muhimu la
kutoa mchango ambalo Taifa linahitaji kuungwa mkono katika kukabiliana
nalo.
Aliuhakikishia Uongozi wa Taasisi hizo kwamba michango hiyo itasimamiwa
vyema kwa ajili ya kuwafika waliohusika kwa kutumia utaratibu
uliotumika wakati wa ajali iliyotokea Mwaka jana.
Alisema licha ya zoezi la uokozi kuwa na gharama kubwa lakini Serikali
inaendelea kutoa huduma zote za mazishi na usafirishaji wa maiti
zinazopelekwa Tanzania Bara ambazo zilipatikana kutokana na ajali ya
Meli ya M.V Skagit hapo juzi.
Aliongeza kuwa shughuli hiyo ikiwemo gharama za vyombo, mafuta, Chakula
na uokozi zinahitaji kuungwa mkono na taasisi na jumuiya ya kiraia ndani
na nje ya Nchi.
“ Serikali imeshachukua jukumu la kuzizika zile Maiti zilizoshindwa
kutambulika hadi sasa, kuzisafirisha maiti tatu hadi Tanzania Bara
pamoja na familia nne wakati maiti moja ya raia wa kigeni bado
haijatambulika”. Alifafanua Balozi Seif.
Alisisitiza kwamba katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo wazamiaji
wa Israel walioko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wameamua kusaidia
kazi ya uokozi kwenya Meli hiyo ili kuendelea kutafuta miili ya Watu
iliyopotea.
Mapema Meneja Msuluhishi wa Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar
{ ZSSF } Ndugu Khamis Phil Phil Than alisema yapo mambo mengi kwenye
tukio hilo la Maafa ambayo yanahitajika kupata msukumo kutoka kwa
Washirika, Taasisi na Jumuiya za Kiraia.
Ndugu Phil Phil alisema mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar umekuwa
mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yake yaliyolenga zaidi
kwenye eneo la Jamii.
Naye kwa upande wake Ofisa
Muandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Tanzania { NSSF }
kutoka Makao Makuu Mjini Dar es salaam Nd. Juma Kimtu alimueleza Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Taasisi hiyo imeamua kutoa mchango
huo baada ya kuona uzito Maafa yaliyotokea ambayo yameigusa Jamii yote.
Ndugu Kimtu alisema Serikali kwa
kuwa ni ya watu haina budi wakati wote kusaidiwa hasa katika masuala
ya Majanga na Maafa ambayo kwa kiasi kikubwa huigusa Jamii yote.
Na
Othman Hamisi Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar
0 comments:
Post a Comment