BAADA
ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, msanii
nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ amesema anafikiria kujitosa
katika muziki wa taarab. Diamond alisema Jijini Dar es Salaam wiki hii
kuwa,amefikia uamuzi huo kutokana na kuvutiwa na muziki huo wa taarab.
Mshindi
huyo wa tuzo mbalimbali za muziki za Kilimanjaro amesema, anajua uamuzi
wake huo utawashangaza mashabiki wengi, lakini ni jambo la kawaida kwa
msanii.
Diamond
alisema hadi sasa anaamini hana mpinzani katika muziki wa kizazi kipya
na hakuna msanii anayeweza kufikia kiwango chake hapa nchini.
Diamond
alisema ameamua kupiga miondoko tofauti ya muziki kutokana na kipaji
alichonacho katika fani hiyo, ambayo imempatia umaarufu mkubwa, Kutokana
na kipaji chake hicho,Diamond alisema hakuna kitu anachoshindwa
kukifanya katika fani ya muziki.
Alisema
bado hajaanza rasmi kupiga muziki wa taarab,na kuwa sasa anafanya
tathmini ya soko la muziki huo ili kuona kama unaweza kumletea mafanikio
kama ilivyo kwa muziki wa bongo fleva.
Alisema
anaweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu anakipaji cha kuimba
nyimbo aina zote, hivyo endapo atafikia muafaka anaweza kufanya muziki
wa taarabu.
Diamond
alikiri kuwa, muziki wa kizazi kipya umemfanya ajulikane sehemu nyingi
duniani, ikiwa ni pamoja na kupata manufaa mbalimbali kimaisha kwa
kuishi kwenye nyumba nzuri na kumiliki magari ya kifahari.
0 comments:
Post a Comment