Warembo wa miss universe Tanzania 2012 wameanza rasmi kambi
katika hoteli yenye hadhi ya kipekee Urban Rose Hotel.Hii ni kwaajili ya
kujiandaa na fainali ya Miss Universe Tanzania 2012 itakayofanyika tarehe 29
mwezi huu wa juni.
Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa
ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake.Mafunzo
hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika nyanja tofauti
ikiwemo TGNP.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia
ni mkurugenzi na muandaaji mkuu wa kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi
Tsehai amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma mbali na kuongeza semina zaidi
ili kuwasaidia warembo lakini pia imefanikiwa kuongeza mikoa ambapo mwaka huu
wameshiriki warembo kutoka mikoa saba ya Tanzania.
Mbali na kutafuta warembo tu bali Miss Universe ni kama chuo
cha kufundisha warembo juu ya kujitambua kama mwanamke na kumpa mbinu
mbalimbali za kimaisha.Vilevile mbali na mshindi kupata nafasi ya kutembea nchi
mbalimbali za kimataifa pia hutoa fursa kwa mshindi kupata nafasi ya kwenda
kusoma nje ya nchi kama vile Marekani kwa kupitia mdhamini wetu mkuu New York
Film Academy’’
Kambi ya Miss universe Tanzania 2012 imekamilishwa na
warembo 20 kutoka mikoa saba ya Tanzania ambayo ni
Dodoma,Arusha,Mwanza,Kilimanjaro,Manyara,Mtwara na Dar es Salaam.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka
2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na
kuliletea sifa taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya
ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa.2008 Miss Universe Tanzania
iliwakilishwa na Amanda Ole sululu,2009 Illuminata James,2010 Hellen Dausen na
Nelly Kamwelu ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yamedhaminiwa na Le
Grande Casino,The citizen,Urban Rose Hotel,Amina Designs,Dodoma Hotel na New
York Film Academy
|
0 comments:
Post a Comment