TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, June 24, 2012

Hali hospitalini Muhimbili, Amana Temeke, M'nyamala baada ya Madaktari kuanza mgomo

1:35 PM
Waandishi wa gazeti la Tanzania Daima Jumapili waliotembelea hospitali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Muhimbili na zile za mkoa ambazo ni Temeke, Amana na Mwananyamala wameshuhudia hali ilivyo hii ni taarifa yao.

Hali ya huduma za afya ni ya kusuasua.

Vitengo vya dharura katika hospitali hizo viliendelea kupokea wagonjwa huku baadhi ya madaktari wakiweka wazi kuwa kuna uwezekano wa huduma hizo kusimama katika muda wa saa 24 kuanzia jana.

Muhimbili

Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wagonjwa walilamikia huduma zilizokuwa zikitolewa huku wengine wakisema wametelekezwa na wauguzi waliokuwa zamu.

Eneo la mapokezi baadhi ya askari walionekana wakiwaeleza wagonjwa waliofika kuwa huduma zimesimama na kuwasihi waondoke eneo hilo.

Mgonjwa mmoja ambaye alionekana kuchanganyikiwa alisikika akisema kuwa alimkabidhi nchi Rais Jakaya Kikwete lakini haieleweki kiongozi huyo anakoipeleka.

“Rais Kikwete nilikukabidhi nchi hii sasa unaipeleka wapi?” alisikika akisema.

John Kobelo, alisema kuwa tangu juzi kijana wake alitakiwa kufanyiwa upasuaji lakini ilipofika jana aliambiwa ampatie mgonjwa wake chakula kutokana na huduma hiyo kutokuwepo.

“Kwa kweli hali inasikitisha na kukatisha tamaa, sijui nchi hii tunaelekea wapi maana viongozi wanaamua kwa makusudi kuchezea uhai wa Watanzania,” alisikika baba mmoja akilalamika.

Tanzania Daima Jumapili ilifika katika wodi ya Sewa Haji na kukutana na mgonjwa ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake lakini alilalamikia kitendo cha madaktari kushindwa kupita zamu kwa siku ya jana huku huduma zikiwa zimezorota.

Katika wodi ya Kibasila gazeti hili lilikutana na baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao walikuwa wakiangaika kumhamisha mgonjwa wao aliyekuwa akilalamika kwa maumivu makali.

Gazeti hili halikuishia hapo kwani lililazimika kufika katika Kitengo cha Mifupa (Moi) ambapo ilikutana na Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Jumaa Almasi, ambaye alisema kuwa kwa jana ilikuwa ni vigumu kuzungumzia mgomo huo kutokana na kuwa siku ya mapumziko.

“Unajua kwa (leo) yaani jana siwezi kuzungumzia mgomo kwa kuwa tuna kliniki mbili za binafsi, labda picha kamili ya kuwepo kwa mgomo tunaweza kuipata kuanzia Jumatatu, kwa vile kuna kliniki zote,” alisema.

Aidha, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alijikuta akishindwa kutokea katika kikao cha waandishi wa habari alichokiita ofisini kwake.

Mwananyamala na Temeke 

Hali ilikuwa si shwari kwani baadhi ya wagonjwa walisikika wakisema kuwa hawajapata huduma na baadhi ya wauguzi wanajifanya kutoa huduma baada ya kuona wanahabari.

Katika Hospitali ya Amana, Tanzania Daima Jumapili ilishuhudia shughuli za matibabu zikiwa zinaendelea ingawa baadhi ya wagonjwa walikuwa wakilalamika kukaa muda mrefu pasipo kupatiwa huduma.

Mmoja wa watu waliokuwa hospitalini hapo aliyempeleka ndugu yake kupatiwa huduma baada ya kupata ajali aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa wamekaa katika eneo hilo zaidi ya saa tatu bila mgonjwa wake kupatiwa matibabu.

“Nipo hapa na huyu afande tumemleta mtu aliyepata ajali maeneo ya Sitakishari lakini hatujahudumiwa mpaka saa hizi sasa sijui ndiyo wanagoma kisirisiri?” alisema mtu huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Katibu wa utawala wa hospitali hiyo, Tunu Mwachale, alisema madaktari waliotakiwa kufika zamu kwa siku ya jana wote walifika na kwamba walikuwa wakiendelea na kazi kama kawaida. 

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz1yhDA52mZ

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA