TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, May 9, 2012

BASI LA KAMPUNI YA MURO INVESTMENT LATEKETEA KWA MOTO MKOANI MOROGORO

2:50 PM


Basi la  Kampuni ya  Muro Investment, T820BEY lillilokuwa klikitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku Mei 8,2012, haikusababisha madhara kwa abiria ispokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo.
http://www.mrokim.blogspot.com/
Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.
 Hapa Matairi yakiteketea kwa moto baada ya basi hilo kulipuka na kuungua lote.
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.
Wakazi wa Maseyu na wasafiri wakiangalia basi hilo likiteketea kwa moto.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA