TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, April 4, 2012

Uongozi wa Jumuiya Ya Ahmadiyya Tanzania Wamtembelea Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dk.Emmanuel Nchimbi

8:21 PM
Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa  Jumuiya ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood Chaundry wakati Uongozi wa Jumuiya  hiyo ulipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam..
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi akimsikiliza Kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood Chaundry wakati walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam (leo)
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi akiongea na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya  ya Ahamadiyya nchini walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salam (leo).Picha Zote na Picha zote na Benjamin Sawe-Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
---
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi ameitaka jamii ya Wahamadiyya nchini  kuendelea na utaratibu wa kuhamasisha amani na kutojihusisha na chuki za kidini.
Waziri Nchimbi ameyasema hayo leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam alipotembelewa na viongozi wa jamii hiyo waliofika ofisini hapo kwa ajili ya kujitambulisha.
Waziri Nchimbi pia ameitaka Jumuiya hiyo kuendeleza vijana  kielimu ili kuwa na taifa lenye vijana wenye maadili mema na hekima kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Kiongozi wa  msafara  huo Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema kuwa Pamoja na mambo mengine jamii  hiyo imekuwa ikijishughulisha na masuala ya maendeleo ya Elimu na Afya  nchini  ambapo kwa upande wa Afya, Jamii hiyo inamiliki hospitali binafsi ya Jamii ya Waislamu ya Wahamadiya  iliyopo mjini Morogoro  na kwa upande wa elimu  wanamiliki  shule ya Sekondari Kitonga iliyopo nje kidogo ya jiji laDar es Salaam.
Aidha, Sheik Chaudhry   amesema kuwa  Jamii hiyo pia inajihusisha na maendeleo ya Michezo mbalimbali ikiwemo riadha, mpira wa miguu, kuvuta kamba kupitia chama chake cha michezo kiitwacho ‘Safina Athletics’ kilichopo jijini Dar es Salaam.
Jamii ya Wahamadiyya iko kwenye zoezi la kujitambulisha katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili kujenga uelewa kwa umma kuhusu kazi wananzozifanya

Na
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA