Uongozi wa Benki ya Azania, (Azania Bank Ltd) unapenda
kuwaaarifu wateja wake na wananchi kwa ujumla ya kwamba
matawi yake mapya ya Arusha City na Moshi mjini sasa yamefunguliwa
ili kutoa Huduma za kibenki.
Tawi la Arusha City lipo Mtaa wa Wapare, jengo la Joshmall
Hotel na Tawi la Moshi lipo Mtaa wa Sokoni. Kwa
Maelezo zaidi piga simu Makao makuu ya Benki Dar es salaam
namba +255 22 2118025/6. Au Tawi la Moshi na +255 27 2754560
na tawi la Arusha City na +255 27 2547354/5.
Pia Benki inapenda kuwaaarifu wakazi wa Mwenge , Dar es salaam
na maeneo ya karibu yake kuwa Tawi letu jipya la Mwenge lililopo
karibu na kituo cha basi Mwenge( jengo la Jamirex) lililofunguliwa
Dec 2011 linaendelea kutoa Huduma zote za Kibenki.
Matawi mengine ya Azania Bank yapo Masdo House, Samora
Avenue, Tegeta na Kariakoo jijini Dar es salaam. Kahama –
Shinyanga, Mbauda jijini Arusha. Mwaloni na Mtaa wa Nkrumah
jijini Mwanza. Karibuni sana mpate Huduma bora za kibenki.
“IMETOLEWA NA
UONGOZI WA AZANIA BANK LTD”.
|
0 comments:
Post a Comment