TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, April 1, 2012

CHANGIENI ZAIDI ELIMU KULIKO HARUSI NA SHEREHE TU

12:12 PM
WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kupenda kuchangia harusi baadala yake wajitokeze kwa wingi kwenye harambee zinazohusu kuchangia elimu kwajili ya kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikali sekta hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa Wapo Mission, Selevester Gamanywa wakati wa uzinduzi wa ‘Siku ya Taaluma’ ambayo itafanyika kila mwaka  katika shule ya sekondari ya Kisukuru Regent, iliyoko Tabata wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
 
 Alisema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiweka kipaumbele katika kuchangia harusi kwa kujua kuwa watakunywa pombe bila kujali hata kama maharusi hawana kitu ambapo kwa wenzao Wakenya hawafanyi hivyo.
 
Gamanywa alisema Wakenya ni taifa pekee ambalo wananchi wake wamekuwa na utaratibu wa kuwachangia watoto ambao wazazi ama ndugu wameshindwa kuwapeleka watoto hao shule kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
 
Aidha, alisema wazazi wanapaswa kutambua kuwa suala la kuchangia elimu ni jukumu la mzazi ambapo kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwajengea uwezo wa kimasomo wanafunzi na kukuza ufaulu wao.
 
“Kuna dhana potofu zilizoibuka miongoni mwa jamii kuwa Kisukuru Regent ni shule ya mtu binafsi kitendo ambacho si kweli bali jamii inapaswa kutambua kuwa mafanikio ya shule hiyo ni ya Wanakisukuru na taifa kwa ujumla”alisema Gamanywa.
 
Gamanywa aliweza kuchangia vitabu 36 vya masomo mbalimbali ambapo baada ya kufanya hivyo wazazi waliyohudhuria uzinduzi huo, kujitokeza na kutoa michango itakayoiwezesha shule hiyo kununua vitabu vya aina mbalimbali  vya kufundishia ambavyo vimekuwavikihitajika kwa kiasi kikubwa katika shule hiyo.
 
Naye Mkurugenzi wa Shule hiyo, Felex Mpiluka alisema siku hiyo,  kutasaidia kuboresha na kunyanyua maendeleo ya ufaulu wa wanafunzi katika shule hiyo

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA