TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, October 14, 2011

MUSTAFA HASSANALI IN AFRICAN FASHION WEEK

1:52 PM
Mustafa Hassanali  Kuzindua  UHURU collection  Africa Fashion Week
Precision Air, kumpeleka Mustafa Hassanali to Afrika Kusini
Ni kwa mara ya Nane kwa Mustafa Hassanali kufanya maonyesho in Afrika kusini.

Ikiwa Tanzania inasherehekea miaka 50 ya UHURU, mbunifu wa kiafrika Mustafa Hassanali’s, atazindua “UHURU” collection ambayo alivutiwa na muonekano wa bendera ya taifa kama iliyopeperushwa Mt Kilimanjaro tarehe 9 Desember 1961 AFI Afrika Fashion Week iliyopo Johannesburg  Afrika Kusini.
“Mkusanyiko huo wa mavazi umehusisha maliasili ya Tanzania, Ambao watu wake ni wenye ukaurimu , nchi yenye utajiri wa maliasili za taifa na  pia ni nchi iliyojengeka na misingi  aloiweka Baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” alisema Mustafa Hassanali
Mkusanyiko huo wa mavazi umepewa jina la UHURU. Na pia haupo tu  kusheherekea miaka   50 ya uhuru wa Tanzania bali uhuru huo kuonyesha uwito, ubunifu na utamaduni.
Kwa kuwa taifa moja,  Mkusanyiko huo wa mavazi  utaonyesha Amani na utengenezaji wa mavazi hayo yataielezea Tanzania kiundani kupitia mbunifu wake kutoka Tanzania Mustafa Hassanali.
Safari ya Mustafa Hassanali ya Afrika kusini imedhaminiwa na  Precision Air, Shirika la ndege lenye ukuaji mkubwa Tanzania ambalo kwa  sasa  linafanya misafara yake   mara 5  kwa wiki  kwa misafara ya Johannesburg.
“Tunafarijika kuwa na  ushirika na Mustafa Hassanali,  ambae atafanya maonyesho  ya mkusanyiko wake wa mavazi kwa mara ya nane Afrika kusini. Muungano wetu mpya unaangalia kutangaza biashara,utalii na utamaduni uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini. alisema  Afisa uhusiano wa Precision air Annette Nkini.
Ikiwa ni mara ya kwanza tena kwa Mustafa Hassanali, Atakuwa ni mbunifu pekee ambae atasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzanian nje ya Tanzania kwa kufanya ufunguzi wa mkusanyiko wake wa Mavazi Afrika kusini.
“Maonyesho ya UHURU collection yatakuwa ni maonyesho yangu ya pili AFI Africa Fashion Week na ya nane kwa jamuhuri ya Afrika kusini, Itakayokuza mahusiano ya pande mbili kati ya Tanzania  na  Afrika Kusini.” Aliongeza Hassanali
AFI Africa Fashion week inamilikiwa na African Fashion Internationals Dr Precious Moloi, itakayofanyika  Sandton Convention Centre kuanzia tarehe  20-22 October. Mustafa Hassanali ndo mbunifu pekee kutoka Tanzania aliealikwa katika wiki ya kujivunia na atafanya maonyesho yake  tarehe 22 October saa 10 jioni

KUHUSU MUSTAFA HASSANALI
Mustafa Hassanali ni mbunifu mjasiriamali anaeamini katika ‘daima sitashindwa’ huku akitumia kipaji chake na ubunifu wake wa mavazi katika kuleta maisha bora ya sasa na ya baadae.
Kazi za mbunifu Mustafa zimekuwa zikithaminika na kuonyeshwa kimataifa, ambapo Mustafa alifanikiwa kuonyesha ubunifu wake katika nchi kama Angola ‘Angola Fashion Business’, FAFA (Festival of African Fashion and Arts in Kenya), Kameruni, Wiki ya Mitindo India 2009, Naomi Campbell’s fashion for relief 2009, Arise Africa Fashion Week 2009, Wiki ya mavazi Durban & Cape town, Vukani Fashion Awards Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashion Festival, Sicily, Italia, M’net Face of Africa, Msumbiji, Uganda, na Wiki ya Mitindo Kenya, ambayo kwa pamoja yamemletea heshima kubwa, ndani na nje ya nchi.
 Ukikutana na Mustafa Hassanali ndipo utajua uwezo wake utokanao na kazi zake,yeye kama yeye anajiamini katika kila anachokitengeneza na anatumia karama na ubunifu wake kutengeneza kilicho bora leo na hata kesho,hasa katika swala zima la mavazi, kwasababu kila akifanyacho hutoka moyoni. Mustafa ni Fashionista wa kweli ndani na nnje

Kwa habari zaidi tembelea tovuti www.mustafahassanali.net
 KUHUSU PRECISION AIR
Shirika la ndege Precision  iimefungua matawi yake mapya  Johannesburg na Hahaya-Comoros miezi miwili ilopita, tarehe 7th Octoba ilianza kuuza share zake  katika  Initial Public Offering (IPO) na ikitarajia kukuza  Dolla za kimarekani  milioni 20 kwa ufungwaji wa IPO tarehe 28th October.

Precision Air  ilitambuliwa na  African Airlines Association (AFRAA) na  Best Scheduled Domestic Airline  kama  shirika la ndege la mwaka  2010 kutoka Tanzania katika  Tanzania Society of Travel Agents (TASOTA) Awards .
 Shirika hili la ndege linamtandao mkubwa nnchini  ikiwemo; Dar es Salaam, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Bukoba, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Ukiachana na safari za mikoani shirika hili lina safari zake pia Nairobi, Mombasa, Entebbe, na kwasasa  Hahaya na Johannesburg.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA