Naibu katibu mkuu wa UM Asha-Rose Migiro
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro ameyataka mataifa kuacha kutegemea misaada. Akiongea kwenye mkutano kuhusu ushirikiano katika maendeleo mjini Luxembourg Bi Migiro amesema kuwa ahadi za kimaendeleo zilizowekwa ni lazima zilindwe na kutimizwa.
Pia amesema kuwa ni lazima kuwe na ushirikiano katika kuhakikisha kuwa misaada inachangia katika maendeleo. Mkutano huo pia unaangazia jinsi ambavyo ushirikiano wa kimaendeleo unaweza kuchangia katika kuafikiwa kwa malengo ya maendeleo ya milenia.
0 comments:
Post a Comment