Na.Mwandishi wetu.
Zoezi la
upasuaji wa kuondoa mfupa wa ziada kwa
Kijana Pascal Issa ambalo liliendeshwa mwanzoni mwa wiki hii, limefanikiwa na
kwamba Pascal anaendelea vizuri na
amelazwa katika hospitali ya CCBRT JIJINI Dar es salaam.
Pascal ambaye alilazwa Jumapili baada ya kupata msaada
kutoka kwa Bw SALUM AWADHI na hospitali
hiyo ya CCBRT anaendelea vizuri na mfupa uliondolewa umepelekwa katika
hopsitali ya Taifa ya Muhimbili kwaajili
ya uchunguzi zaidi.
Kwa upande wa Madaktari waliendesha upasuaji huo uliochukua
Saa NNE wamesema, upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa na kwamba
Pascal ataendelea kubaki hospitali hapo kwa uangalizi zaid mpaka atakapojiskia
vizuri sambamba na kusubiri majibu ya Mfupa huo uliotolewa .

0 comments:
Post a Comment