This photo of Hotel South Beach Resort Dar Es Salaam is courtesy of TripAdvisor
This photo of Hotel South Beach Resort Dar Es Salaam is courtesy of TripAdvisor
This photo of Hotel South Beach Resort Dar Es Salaam is courtesy of TripAdvisor
Ni ya mwekezaji anayedaiwa kuua raia kwa kumchoma
Wakazi
wa Mjimwema Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam wamekuja juu na kuipa
Serikali siku saba iwe imefunga Hoteli ya Kitalii ya South Beach na
kumuondoa mwekezaji anayetuhumiwa kufanya mauaji ya mwenzao, Lila
Hussein (34), vinginevyo wataitisha maandamano makubwa ya vijana ili
kuichoma moto.
Hatua
hiyo ya wananchi imefikiwa siku chache baada ya kijana huyo ambaye ni
mkazi wa eneo hilo kudaiwa kuchomwa moto na mmiliki wa hoteli hiyo,
Salim Chipata (53), na kumsababishia majereha mwilini mwake kabla ya
kifikwa na mauti mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa amelazwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Wakizungumza
katika kikao cha pamoja na uongozi wa mtaa wa Mjimwema kilichofanyika
jana Kigamboni, wananchi hao walisema wamechoshwa na vitendo vya
kikatili vinavyofanywa na mwekezaji huyo ambavyo vinakiuka haki za
binadamu.
“Kila
mara tunaokota maiti jirani na hoteli hii ya South Beach na sisi
tunadhani huyu mmiliki wake anajua vifo hivi vinatokana na nini, hivyo
hili tukio la sasa la mauaji ya kuchomwa moto hatutakubali lipite hivi
hivi,” alisema mmoja wa wakazi hao.
Akizungumza
katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wananchi wa eneo hilo pamoja na
maofisa wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) cha jijini Dra es
Salaam, Ali Seleiman Mwambogo (83), alisema suluhisho la matatizo
yanayoendelea kutokea katika hoteli hiyo ni kuifunga.
Alisema
kama Serikali haitasikiliza kilio chao na kuifunga hoteli hiyo, wao
watahamasisha vijana ili waivamie na kuichoma moto kwa madai kuwa
mmiliki wake ameua kijana wao ambaye hakuwa na hatia yoyote.
Alilalamika
kuwa Serikali ina kawaida ya kuwasikiliza wawekezaji kuliko wananchi
wake na kwamba kama itatokea ikafanya hivyo ijiandae kushuhudia maafa
makubwa katika eneo hilo.
Alishauri
kuwa licha ya hoteli hiyo kufungwa, pia itaifishwe na kupewa mtu
mwingine ambaye atakuwa na moyo wa kibinadamu anayeweza kushirikiana na
wananchi wanaoizunguka eneo hilo.
Mkazi
mwingine wa eneo hilo, Mohamed Athumani (75), akizungumza katika kikao
hicho alisema lazima walipize kisasi kwa kuwa ndugu yao ameuawa kikatili
kwa kuchomwa moto na mwekezaji huyo bila hatia.
Aliitaka Serikali itafute mahali pa kumpeleka mwekezaji huyo vinginevyo wananchi wataungana na kwenda kuiteketeza kwa moto.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mjimwema, Mwinyi Baishi,
aliungana na wananchi wake na kuiomba Serikali kuwasaidia kwa kuifunga
hoteli hiyo ili kuepusha maafa makubwa ambayo yamepangwa kufanywa na
wananchi baada ya siku saba kupita.
Alisema
baada ya mwekezaji huyo kudaiwa kusababisha mauaji hayo, Serikali
ifuatilie ili kuona kama bado ana uhalali wa kuendelea kuwa mwekezaji
anayemiliki hoteli ya kitalii.
Hivi
sasa hoteli hiyo inalindwa na askari polisi wenye silaha baada ya
mmiliki wake kushikiliwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za kusababisha
mauaji ya Lila.
Anadaiwa
kummwagia petroli Lila na kumchoma moto baada ya kumtuhumu kuzamia
kwenye muziki wakati wa usiku katika hoteli hiyo bila kutoa malipo.
Chipata alipandishwa kizimbani juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kumchoma moto Lila.
Mtuhumiwa
huyo mkazi wa Mikocheni A, alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Temeke, Khasim Mkwawa, akiwa pamoja na mshtakiwa mwenzake,
John Mwangiombo (32), kujibu mashtaka hayo.
Mwendesha
Mashtaka, Inspekta wa Polisi, Dustan Kombe, aliiambia mahakama hiyo
kuwa Aprili 10, mwaka huu, saa 6:30 usiku eneo la Mjimwema Kigamboni,
washtakiwa walishirikiana kumpiga na kumchoma Lila na kumsababishia
kifo.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment