Msanii wa muziki wa injili nchini Miriam Lukindo akiwa katika pozi
Msanii wa muziki wa injili nchini Miriam Lukindo akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii.
MSANII
wa muziki wa injili nchini Miriam Lukindo Mauki anatarajia kuzindua
video ya albamu yake ya pili iitwayo "Ni asubuhi", uzinduzi huo
utafanyika Aprili 10 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari asubuhi hii, Miriam alisema ili kupamba uzinduzi
huo wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili watasindikiza.
Aliwataja
wasanii hao kuwa ni pamoja Christina Shusho, Jackson Bent, Martha
Mwaipaja, The Voice Band, The Whispers, Makuti Kawe na Marion Shako
kutoka Nchini Kenya.
Nyimbo
zilizomo kwenye albamu hiyo ni pamoja na Ni asubuhi, Sema na Moyo
wanghu, Anasikia,Amefanya, Wewe ni sababu, Mungu yu Mwema, Twende na
Yesu na Amen Amen.
Aidha, kiingilio katika uzinduzi huo kimepangwa kuwa ni sh.10,000 kwa viti maalum na 5,000 kwa viti vya kawaida.


0 comments:
Post a Comment