TIMU ya
soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imefuzu kushiriki
fainali zijazo za Olimpiki baada ya wapinzani wao, Sudan kujitoa katika
mashindano hayo.
Twiga
Stars ilikuwa ishuke mechi ya kwanza Aprili 30 huko Sudan na kurejeana
na wapinzani wao hao waliojitoa hapa nyumbani Mei 14 hapa jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Angetile Osiah, alisema kuwa wamepokea taarifa kutoka katika
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kwamba Sudan haitaweza kushiriki
michuano hiyo na hivyo kuipa nafasi Twiga Stars kufuzu fainali hizo kwa
mara ya kwanza.
Osiah
alisema kuwa kutokana na taarifa hizo sasa timu hiyo iliyokuwa imeanza
mazoezi chini ya Kocha wake, Mkuu, Boniface Mkwasa, itavunja kambi na
baadaye itatafutiwa mechi mbalimbali za kirafiki ili kujiweka imara na
michuano hiyo itayoshirikisha timu nane katika hatua hiyo ya fainali.
Sudan
nao walifuzu kucheza hatua ya pili baada ya wenzao wa Kenya kujitoa
katika hatua ya kwanza kutokana na kutokuwa na timu ya wanawake.PICHA NA JANE JOHN.
|
0 comments:
Post a Comment