*NI KUKAMILIKA MRADI WA MAJI SINGIDA
*PROF. MWANDOSYA AAHIDI KUTEMBELEA
Na.Mwandishi wetu, Dodoma.
Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohamed Dewji (MO) leo amembana
Naibu Waziri wa Maji Injinia Gerson Lwenge juu ya kukamilika kwa mradi wa maji.
Katika swali lake nyongeza Mh. Dewji amesema tatizo la maji
katika Jimbo la Singida Mjini ni kubwa na kwamba wananchi wamekuwa wakihangaika
kutafuta maji safi na salama.
Hata hivyo, amesema kuwa kuna mradi wa maji ambao
unafadhiliwa na Benki ya BADEA, lakini umechukua muda mrefu kukamilika kwake na
kutaka maelezo juu ya hatua zinazochukuliwa.
Akijibu swali hilo, Injinia Lwenge amekiri kuwepo kwa mradi
huo na kusema kuwa serikali inaendelea kutekeleza ili kuhakikisha wananchi
wanapata maji safi na salama.
Amesema kuwa mradi huo uko katika hatua nzuri ya kukamilika
na kumtaka Mh. Dewji na wananchi wa Singida kuwa subira.
Baada ya jibu hilo la serikali, Waziri wa Maji Profesa Mark
Mwandosya alisimama kuomba kutoa ufafanuzi kuhusu swali la Mh. Dewji, ambapo amesema
kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge lijalo, atakwenda kukagua mradi huo.
|
0 comments:
Post a Comment