Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na watoto, Mh. Ummy Ally Mwalim,
jana alipata muda wa kutembelea maonyesho yanayoendelea ya Harusi ndani
ya ukumbi wa Diamond Jubilee jana jioni.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda yote yanayokadiriwa kuwa zaidi ya
50 ya wajasiriamali tofauti tofauti wanaojihusisha na masuala ya
harusi, Naibu waziri alimsifu muaandaaji wa maonyesho hayo, ambae pia
ni mbunifu mahiri wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali kuwa ni
mjasiriamali anayejituma na ni mfano wa kuigwa.
“kwa
kweli Mustafa amefanya kitu cha kipekee sana, naa ni mfano wa kuigwa,
hii inawapa wafanyabiashara husussani wale wa mapabo na keki kuweza
kujitangaza na kujifunza mengi wao kwa wao” alisema mheshimiwa Waziri.
Naibu
waziri ambae aliweza kupata wasaa wa kubadilishana mawazo na wadau na
washiriki wa maonyesho hayo ambao walimpoke kwa furaha huku wakimpa
zawadi mbalimbali, aliwasihi na kuwapa moyo wa kuendelea kujituma kwa
ari bila kuchoka ili kujipatia kipato na kuwapa huduma wananchi kwa
uzuri na usasa zaidi.
Nae
muaandaji wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali, ambae ndie aliyekuwa
mwenyeji wa mh. Naibu waziri, alisema kuwa maonyesho ya mwaka huu
yamekuwa ni ya aina yake kutokana na kujipanga kwa timu nzima ya
uandaaji, huku baadhi ya mambo yakiwa yameongezeka tofauti na mwaka
jana.
“mwaka
huu sambamba na maonyesho haya, tumeweza pia kuzindua jarida ambalo ni
mahususi kwa masuala ya Harusi, hii ni kwa mara ya kwanza Tanzania
kuwa na jarida la namna hii ambalo litatoka mara nne kwa mwaka, pia
tumeweza kuwa na midahalo mbalimbali ya wazi ya kuelimisha juu ya
masuala ya Harusi na ndoa” alisema Hassanali.
Akizungumzia
kuhusu muitikio wa watu kuja kutembela maonyesho hayo, Mustafa
Hassanali alisema kuwa “kwa mwaka huu, namba ya washiriki imeongezeka
zaidi ya ile ya mwaka jana, huku watu wanaokuja kutembelea
maonyesho haya pia inaongezeka siku hadi siku, jana walikuwa wachache,
na hii ilitokana na kuwa jana ilikuwa ni siku ya kazi, ila leo
kwakweli tumepokea watu wengi sana, na bado tunawaomba watu wajitokeze
kwa wingi kwa siku ya kesho ambao ndo tunafunga rasmi maonyesho haya.”
Alimalizia kuzungumza Hassanali.
Hii
ni mara ya pili kwa maonyesho haya ya Harusi kufanyika nchini, huku
yakiwa na matarajio ya kuishirikisha mikoa mingi zaidi nchini kwa miaka
ijayo, tofauti na mwaka huu ambapo mikoa ya Arusha, Zanzibar na Dar es
salaam tu ndio iliyoshiriki.
0 comments:
Post a Comment