Katibu
wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema Khatib akiwa katika viwanja
vya Bunge jana mchana alianza kujisikia vibaya na kusaidiwa na watu
waliokuwa karibu ambao waliompeleka katika zahanati.
Alisema baadaye mbunge huyo alipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Alisema kuwa Khatib alijisikia vibaya baada ya presha kushuka.
Kwa
upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Godfrey Mtey,
alithibitisha kupokelewa kwa mgonjwa huyo na kwamba hali yake ilikuwa
inaendelea vizuri.
“Hakuanguka
bali alianza kujisikia kuchoka na kujipeleka mwenyewe katika zahanati
ya Bunge na sisi huwa hatupuuzi kitu tukaamua kumpumzisha ili aweze
kufanyiwa uchunguzi,” alisema na kuongoza:
“Anaendelea vizuri hakuna haja ya kuwa na wasiwasi bado tunamuangalia afya yake.”
Alisema mbunge huyo alipelekwa katika hospitali hiyo jana saa 7.00 mchana na kwamba hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.
Hata hivyo, waandishi wa habari hawakuruhusiwa kwenda kumuona baada kuelezwa kuwa alikuwa akihitaji mapumziko.
0 comments:
Post a Comment