Meneja
Uhusiano na Mawasiliano ya Umma wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Editha Mushi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni nane
Mwenyekiti Wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(Taswa), Juma Pinto Dar es Salaam jana kwa ajili ya tamasha la vyombo
vya habari Jumamosi wiki hii, ambapo TBL imedhamini kwa sh. milioni
50.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Maulid Kitenge
Mwenyekiti
wa TASWA akizungumza (katikati) Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya Umma
(TBL), Editha Mushi na Makamu Mwenyekiti TASWA, Maulid Kitenge.
BENDI
ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ itatumbuiza kwenye bonanza la vyombo
vya habari litakalofanyika Jumamosi wiki hii Coco Beach, Dar es Salaam.
Pia
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kitatumia
bonanza hilo kutoa tuzo maalum kwa waandishi wa habari ambao hivi sasa
wamepata nafasi katika vyama vya michezo ama taasisi nyingine mbalimbali
kubwa za kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa TASWA, Juma
Pinto alisema maandalizi ya bonanza hilo litakalohudhuriwa na watu
1000, kati yao 800 wakiwa ni kutoka vyombo mbalimbalimbali vya habari
yanaenda vizuri.
Alisema
bonanza litaanza saa nne asubuhi hadi saa mbili usiku na kwamba vyombo
mbalimbali vya habari vimealikwa na kuwa kila chombo kinatakiwa
kuthibitisha michezo kitakayoshiriki kwa Katibu Mkuu wa TASWA kabla ya
Alhamisi saa tano asubuhi ili ratiba ipangwe.
Alisema
michezo mbalimbali itashindaniwa ambayo ni soka ya ufukweni (wanaume),
netiboli (wanawake), wavu (jinsia zote watachanganyika), mbio za magunia
(wanawake na wanaume), mbio meta 100, kuruka kichura (wanawake na
wanaume) na kuvuta kamba (jinsia zote watachanganyika) na kucheza muziki
(wanawake na wanaume).
Alisema
michezo yote itakuwa na zawadi ya vikombe isipokuwa kucheza muziki
zawadi yake ni fedha taslimu, ambayo itatangazwa Alhamisi.
Kuhusiana
na tuzo, Pinto alisema Kamati ya Utendaji ya TASWA imekubaliana kuwa
wapo waandishi ambao wamepata nafasi mbalimbali kwenye taasisi tofauti,
lakini kwa kutambua mchango wao, TASWA imeamua kuwapa tuzo.
“Idadi
yao ni kubwa sana, lakini tumeamua kwa vile sisi tuliingia madarakani
Agosti mwaka jana, basi waandishi wote ambao wapo kwenye taasisi
nyingine, lakini walikuwa waandishi wa habari mpaka wanapata nafasi hizo
tutawapa tuzo.
“Mfano
ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Ofisa Habari wa TFF, Boniface
Wambura, Wabunge Lucy Mayenga, Juma Nkamia, Esther Bulaya na wengine
wengi.
“Nitoe
angalizo kuwa tunawapa tuzo maalum ambayo itaonekana siku hiyo wale
waliopata mafanikio hayo kuanzia Agosti mwaka jana, orodha kamili
tutaitoa Alhamisi kwenye mkutano wetu na wana habari.
“Si
waandishi wa michezo tu, bali hata wa siasa, uchumi na mambo mengine,
lakini wawe katika vyama ama taasisi za kitaifa, si klabu ama taasisi
ndogondogo,” alisema Pinto.
Naye
Meneja Uhusiano na Mawasiliano ya Umma wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), ambao ndio wadhamini wa bonanza hilo, Edith Mushi alisema
udhamini wao unagharimu kiasi cha sh. Milioni 50 na kuwa kampuni yake na
TASWA zimegawana majukumu kwa bonanza hilo.
Jana TBL ilikabidhi mfano wa hundi y ash. Milioni nane, ambayo TASWA ndiyo itayashughulikia kwa ajili ya bonanza hilo, huku mengine ikiwemo masuala ya vinywaji yakifanywa na TBL.
“Kama
mnavyofahamu TBL imekuwa karibu na waandishi wa habari katika masuala
mbalimbali na ndiyo sababu imeweka nguvu zake kwenye bonanza la mwaka
huu.
“TBL
itahakikisha bonanza la mwaka huu linafana na linakuwa la aina yake
kuanzia katika michezo, vinywaji na vyakula ili kila mmoja aamini kwamba
kweli limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji.
“Tunawaomba
waandishi wajitokeze kwa wingi huku tukiamini kwamba kila mmoja
atafurahi siku hiyo, maana lengo ni kuwakutanisha pamoja watu wa tasnia
hii na kubadilishana mawazo na pia kupongezana kwa kazi ngumu
mnayoifanya,” alisema.
Naye
Meneja wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Hassan Rehani alisema
bendi yake ipo imara na kuwa waandishi watakaofika siku hiyo watafurahi
zaidi.

0 comments:
Post a Comment