TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, March 9, 2011

MEJA JENERALI (MSTAAFU) MWAKITOSI AZIKWA LEO KISUTU, MIZINGA 13 YARINDIMA

11:29 PM
MAOFISA wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakibeba jeneza lenye mwili wa Meja Jenerali Mstaafu,  Jumanne Mwakitosi, wakati wa mazishi yaliyofanyika leo, kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. Meja Meja Jenerali Mwakitosi alifariki juzi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Wanajeshi wakilifikisha jeneza lenye mwili kwenye eneo la kaburi
Kisha mazishi kwa mujibu wa dini yake ya Kiislamu yakafanywa. Hapa wahusika wameingia kaburini tayari kuzika.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ,  Abdulrahman Shimbo (kushoto) akiungana na waombolezaji wengine kuomba dua baada ya mazishi hayo. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga, Meja Jenerali Mstaafu, Saidi Kalembo.
Kisha JWTZ wakatoa heshima ya Kijeshi kwenye kaburi
Askari wa JWTZ wakirindimisha mizinga 13 kwa heshima ya kijeshi ya mazishi hayo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi (kushoto), Waziri wa Ulinzi Dk. Huseein Mwinyi na Waziri wa mambo ya Ndani wa zamani, Lawrence Kego Masha (kulia) walikuwepo kwenye mazishi hayo, bila shaka hapa walikuwa wakiteta jinsi Marehemu alivyokuwa mtu muhimu katika jamii.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA