 |
| Mbunge wa Viti Maalum (CCM). Vicky Kamata akisalimiana na Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa baada ya kuiba wimbo wake, wabla ya uzinduzi wa
albamu hiyo. Kulia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanaisa la Ufufuo na Uzima,
Josephati |
 |
| Lowassa akieleza yake machache na kuongoza kuimba wimbo wa kumtukuza
Mungu, kabla ya kuzindua rasmi albamu hiyo na kuendesha harambee ya
uchangiaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto yatima Kiluvya |
 |
| KIONGOZI wa Bendi ya muziki wa Injili ya Mwanamapinduzi, Mchungaji
Maximilian Machumu, akimkabidhi CD, DVD NA Kanda za albamu ya 'Bonde la
kukata maneno', Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wakati wa
uiznduzi wa albamu hiyo, uliofanyika juzi, katika ukumbi wa Diamond
Jubilee, Dar es Salaam. Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi huo, alichangia sh. milioni moja. Katikati ni, Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (GCTC Josephat Gwajima. |
BENDI
ya muziki wa injili ya Mapinduzi, imevuna jumla ya sh. milioni 40,
katika uchangishaji fedha uliosimamiwa na Waziri Mkuu wa zamani Edward
Lowassa, kwenye uzinduzi wa albamu ya 'bonde la kukata maneno' juzi
katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Kabla ya kuanza harambee
ya uchangiaji fedha hizo, ambazo zitatumika kwa ujenzi wa kituo cha
yatima, eneo la Kilivya wilayani Kinondoni, Lowassa alichangia Sh.
miliomi moja, na kufuatiwa na wadau wengine akiwemo Mbunge wa viti
maalum (CCM) Vicky Kamata aliyechangia Sh. 300,000.
Akizungumza katika uzinduzi huo,
Lowassa alisema, umefikia wakati ambao Watanzania sasa waachane na
malumbano na kutupiana maneno yasiyojenga, dala yake, wajikite katika
kufanya mambo yenye tija ikiwemo kumcha Mungu ambaye ndiye mwenye uwezo
katika kila jambo.
Mapema, Ofisa Mtendaji Mkuu wa
kampuni ya Rudisha Music, iliyoaandaa uzinduzi wa albamu hiyo, Frederick
Fussi alisema, lengo ni sehemu ya pamato ikiwa ni pamoja na mnada wa
DVD, VCD na Kanda yatatumika kujenga kituo hicho cha yatima ambapo
ujenzi huo umekadiriwa kuhitaji sh. milioni 120.
Uzinduzi uliambatana na burudani
za sarakasi na tumbuizo za muziki wa injili kutoka kwa Kamata na
vikundi kadhaa vya muziki huo na kufuatia na Maximilian mwenyeye na
kundi zima la Mapinduzi, kupanda jukwaani kuzindua rasmi almabu yao,
hatua iliyosababisha mamia ya watu waliohudhuria kupata burudani murua
kutokana na umahiri ulioonyeshwa.
0 comments:
Post a Comment