![]() |
| Mchungaji Ambikile Mwasapile akiwaelezea watu kuhusu dawa hiyo inavyotibu magonjwa mbalimbali |
![]() |
| huu ndo mti wenyewe wa mugariga |
![]() |
| dawa ikichemshwa ikiwa ni hatua ya kuiandaa |
![]() |
| watu kibao kutoka sehemu mbalimbali wakisubiria dawa |
MAELFU WAFURIKA LOLIONDO KUPATA DAWA KWA BABU, WATU KADHAA WAHOFIWA KUFARIKI DUNIA WAKIWA KATIKA FOLENI
Na Woinde Shizza
Maelfu ya watu wanazidi kumiminika katika wilaya ya ngorongoro kata ya digodigo katika kijiji cha Samunge huku baadhi yao wakiwa mahututi sana na wengine Kupoteza maisha kutokana na msongamano wa watu na kuchelewa kupata huduma.
Wananchi
hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali huku wengine wakitoka nchi
za jirani ikiwemo nchi ya Kenya na Uganda wamemiminika katika kujiji
hicho wengi wao wakiwa wanataka dawa kutoka kwa mchungaji mstaafu,
Ambilikile Mwasapile, ambaye anatibu maradhi ambayo yanawasumbua kwa
muda mrefu na ambayo walikuwa hawategemei kama wangekaa wapate dawa
zake.
Pamoja ya kuwa watu wengi wanazidi kumiminika wilayani ngorongoro kupata matibabu kwenye nyumba ya mchungaji huyo lakini pia mamia
ya watu wengine wamekwama jijini Arusha na katika eneo la Mto wa Mbu
kutokana na kukosa usafiri wa kuweza kuwafikisha nyumbani kwa mchungaji
Mwasapile huku wengine waliofika katika nyumba ya mchungaji huyo na
kupata huduma wakiwa wanashindwa kurudi makwao kutokana na kukosa
usafiri mara baada ya magari ambayo yaliwaleta kuondoka kutokana na
kukaa muda mrefu.
Mbali
na kuachwa na magari pia maelfu ya watu ambao wanaenda kupata matibabu
wengi wao wamekuwa wakipata shida sana kwa ajili ya malazi na chakula
kwani wanalazimika kulala kwa muda mrefu kutokana na wingi wa watu
wanaowakuta hali inayowasababishia wananchi hao kukaa kwa muda hata wa
siku tano na kuendelea na kulazimika kulala chini na wengine kupata
chakula kwa njia ya shida sana hali ambayo inaleta hofu kubwa kwani watu
wengi wanaofia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza tokea kuotokana na
msongamano huo wawatu wengi .
Pia
katika msongamano huo wa watu umeleata madhara kwani pia kuna baadhi ya
wagonjwa ambao wameletwa wakiwa mahututi wamefariki kutokana na
kuchelewa kupata huduma mapema na mpaka kufikia Juzi watu watu saba
walikuwa wamefariki dunia akiwemo mtoto mmoja.
Mwandishi
wa habari hizi mbali na kushuhudia maiti hizo bado aliwaona wagonjwa
wengi ambao walikuwa wameletwa kupata huduma huku wengine wakiwa
wanaonekana kufika sehemu hiyo wakiwa na dripu mikononi na wengine
wakiwa hawajiwezi kabaisa.
Pamoja
ya kuwa mchungaji Mwasapile alijitaidi sana kuhudumia wagonjwa ambao
walifika sehemu hile lakini haikusaidia nahadi kufika jana jioni ilibidi
waongeze wachungaji wengine wawili kumsaidi mchungaji huyu ili kuweza
kupunguza watu kwani kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wagonjwa
wanazidi kumiminika zaidi .
Mchungaji
Mwasapile alipoongea na gazeti hili alisema kuwa analazimika kufanya
kazi kwa muda mrefu ili kuweza kuwahudumia wagonjwa ambao wanafika hapo
na pia alibainisha kuwa ameoteshwa kuwa watu watu
bado wanaongezeka na wanatoka katika nchi mbalimbali na mabara
mbalimbali hali ambayo itafikia mahali hata itamgarimu mtu kuchukua hata
waki tano kupata huduma.
Mchungaji huyo alisema kuwa yeye mungu alinena naye kwa njia ya ndoto kuhusiana na dawa hiyo
inayotokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula maarufu cha Twiga,
tangu mwaka 1991 lakini alianza kutibu ugonjwa mmoja ambao ni wa ukimwi
tu na ilipofika mwaka jana mungu alinena naye tena na ndipo alimwambia
dawa hiyo inatibu pia hayo magonjwa mengine.
“na mungu aliponiotesha aliniambia kabisa na mtu ambaye nitaanza kumtibu na kweli alikuja mama mmoja wa
hapa hawa kijijini na nikampa akapona baada ya mama huyo walikuja
wanafunzi wawili pia niliwatibu nao wakapona na ndipo wakaanza kueneza
na watu wakaja nikawapa na wamepona kabisa”alisema Mwasapile
Alisema
kuwa dawa hii ainyeki mara mbili tiba yake ni mara moja tu na alisema
kuwa kwa upande wa watu wenye ugonjwa wa HIV itanawatibu baada ya siku
21 ambapo alifafanunua kuwa akienda kupima mara ya kwanza ataonekana
anavyo ,mara ya pili ataonekana anavyo yaani wiki ya pili na akienda
wiki ya tatu ambayo itakuwa ni baada ya wiki 21 atakuwa hana kwa upande
wawatu waenye kisukari alisema kuwa wao wanapona baada ya kunywa iyo
dawa tu.
"Wanaopona
HIV waache kujiingiza katika matendo ya kupata maambuki kwani
hawatapona tena, Hii dawa sio kinga ni tiba na hairuhusiwi kunywa zaidi
ya kikombe kimoja,"alisema Mchungaji Mwasapile.
Kwa
upande wa msaidizi wa mchungaji huyo(Babuu), Marko Nedula alisema kuwa
watu wengi wanaofika kupata huduma kwa mchungaji huyo wanatoka nje ya
wilaya ya Ngorongoro pamoja na wengeji ambapo alifafanua kuwa awali
wenyeji walikuwa wanazarahu dawa hiyo na kusema kuwa hawamuamini lakini
baada ya kuona wageni wengi wanajitokeaa kunda kunywa ndio na wao
wameanza kujitokeza kwa wingi.
Pia
alisema kuwa anapenda kuwasihi watu ambao wanawaleta wagonjwa waho
kujitaidi kuwaleta wagonjwa wakiwa angalau wananafuu kwa kiasi na
wasiwachukuwe wagonjwa wao hospitali wakiwa mahututi kwani kwa sasa ivi
msongamano wawatu umezidi hali ambayo inafanya kuchelewa kuwahudumia .
”unajua napenda kuwaambia wasiwachukuwe wagonjwa wao wakiw amahutiti kwani ndo inaweza kuwasababishia mathara ikiwemo wakiwaleta hapa wanaweza kuwapoteza kwani wakija wanakuta kunawagonjwa wengine wamekuja na niwagonjwa zaidi hadi huduma kuwafikia itachukuwa mda kitu ambacho kama alimchukuwa mgonjwa mahututi hospitalini anaweza kuupoteza maisha na kama wata wachukuwa basi wabebe dawa ambaozo zitawasaidia hadi pale mchungaji atakapo wafikia kuwapa huduma.
”unajua napenda kuwaambia wasiwachukuwe wagonjwa wao wakiw amahutiti kwani ndo inaweza kuwasababishia mathara ikiwemo wakiwaleta hapa wanaweza kuwapoteza kwani wakija wanakuta kunawagonjwa wengine wamekuja na niwagonjwa zaidi hadi huduma kuwafikia itachukuwa mda kitu ambacho kama alimchukuwa mgonjwa mahututi hospitalini anaweza kuupoteza maisha na kama wata wachukuwa basi wabebe dawa ambaozo zitawasaidia hadi pale mchungaji atakapo wafikia kuwapa huduma.
Pia
gazeti hili lilibahatika kuzungumza na mmoja wa wanakijiji wa kijiji
hicho aliyejulikana kwa jina la Ana Mateyo ambaye yeye alisema kuwa
wamefurahia sana dawa hiyo kupatikana katika kijiji chao kwani wamekuwa
wakifanya biashara kwa kasi kubwa mno na kusema kuwa wamekuwa wakipata
hela kwani soda tu wamekuwa wakiuza shilingi 1000 huku maji ya kunywa
wakiwa wanauza shilingi 2000.
Alisema
kuwa pia wamefurahia sana kwani hata wao wenyewe kupitia babu huyo
wanaweza kujikwamua katka maisha magumu kwani wanajiingizia kipata kila
siku na wanafanya biashara kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa
upande wa mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maramu Juma
alisema kuwa yeye anafurahi sana kwani alifaika ngorongoro akiwa anaumwa
na amebebwa lakini tangu anywe iyo dawa amesisimama mwenyewe na
anatembea kitu ambacho amemshukuru mungu kwa kumleta mtumishi huyu
katika nchi ya Tanzania.
Baadhi ya wagonjwa ambao waliohudhuria katika kujiji hicho waliomba
jeshi la polisi mkoani Arusha kuongeza askari wa kutuliza gasia ambao
wataweza kuwapanga watu na kuwaelekeza kufuata utaratibu uliowekwa ili
kuweza kusaidia vurugu zisitokee.
Walisema
kuwa mgambo ambao wapo katika eneo hilo hawawezi kutosha kutuliza
vurugu hizo kwani jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wananchi
wanavyozidi kuongezeka na wakija wale waliochelewa huleta fujo na kutaka
kuanza kupewa dawa wao badala ya wale walio tangulia.
“tunaomba
jeshi la polisi liongeze idadi ya askari waweze kusimamia utaratibu
kwani muda mungine babu anashindwa fanya kazi kutokana na vurugu unakuta
mtu amekuja hapa leo na kuna mungine kaja juzi yule wa leo ataki
kufuata utaratibu uliowekwa analeta fujo kitu ambacho kinaleta ata
uvunjifu wa amani “alisema mmoja wawagonjwa aliyejulikana kwa jina la
Godfrey Lymo.




0 comments:
Post a Comment