TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, February 3, 2011

NYAYO ZA BINADAMU WA KALE KUFUKULIWA HIVI KARIBUNI

10:24 PM


NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO

Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige amesema Wizara yake inatarajia kufukua Nyayo za Binadamu wa kale maarufu kama Zamadamu zinazopatikana katika eneo la Laetoli mkoani Arusha ifikapo tarehe 7 Februari, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri huyo amesema kuwa ufukuaji wa nyayo hizo utafanyika kwa muda wa wiki mbili ambapo takribani milioni mia mbili zinatarajiwa kutumika katika ufukuaji huo.

“Zoezi hili la ufukuaji wa nyayo za Zamadamu litagharimu fedha za kitanzania milioni mia mbili ambazo mpaka sasa zimekwisha anza kutumika na tayari baadhi ya wafanyakazi wameshatanguli katika eneo husika.” Amefafanua Maige.

Waziri Maige amesisitiza kuwa Kukamilika kwa shughuli hii ya ufukuaji kutakuwa mwanzo mzuri wa maandalizi ya kufukua nyayo zote hapo baadaye ambazo zitatafutiwa mazingira mazuri ya kuhifadhi nyayo hizo bila kuharibika.

Nyayo za zamadamu wenye umri wa miaka milioni 3.6 zilivumbuliwa na mtafiti maarufu Dkt mary Leakey mwaka 1978 katika eneo la Engarusi huko Laetoli ndani ya hifadhi ya Ngorongoro na nyayo hizo zimehifadhiwa kwenye mwamba wa Volcano.

Nyao hizo zilizotunzwa kwenye mwamba wa Volcano sio tu kwamba zinatunza kumbukumbu za aina ya wanyama na ndege walioishi wakati huo bali pia ni kielezo muhimu kinachoonesha kuwa kwa kipindi hicho binadamu alikuwa anasimama na kutembea kwa miguu miwili.

Warsha ya Sheria ya Utekelezaji wa Kanuni za Udhibiti wa Kemikali

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Edwin Mungongo akifunguwa Warsh ya Wasimamizi wa Utekelezaji wa Kanuni ya Udhibiti wa Kemikali zinazomongonyoa Tabaka la Ozoni kulia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Julias Ningu Huko Ubungo Plaza Mijini Dar es Salaam
Baadhi ya Washiriki wa Warsha Wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mkurugenzi Msaidizi Dk Edwin Mungongo (PIchani hayupo) Sheria ya Utekelezaji wa Kanuni za Udhibiti wa Kemikali Zinazomong'onyoa Tabaka la Ozoni Huko Ubungo PIaza Leo (Picha na Ali Meja}

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA