TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, February 20, 2011

NDEGE (FLY540) YAPATA AJALI NA KUANGUKA CHINI!

11:13 PM
Pichani ni Ndege aina ya Fokker 27 namba 5X-FFD ikiwa imeanguka ilipokuwa ikiajiandaa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Wilson uliopo jijini Nairobi kutokana na hitilafu.

Na.Mwandishi wetu

Wakati Shirika la Ndege la fly540 Tanzania likipanga kupanua wigo wa utoaji huduma katika maeneo mbalimbali nchini baadhi ya abiria wamepata wasiwasi kuhusu usalama na ubora wa ndege za abiria za shirika hilo.

Wasiwasi huo unafuatia ajali ya moja ya ndege hizo iliyotokea Januari 28 mwaka huu jijini Nairobi, Kenya ambapo ndege aina ya Fokker 27 namba 5X-FFD kuanguka ikiajiandaa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Wilson uliopo jijini Nairobi kutokana na hitilafu.

Mmoja wa wateja wa ndege za shirika hilo ambalo awali lilijikita katika kusafirisha watalii katika hifadhi zilizopo nchini na nje ya nchi amesema ingawa wamekuwa wakitumia muda mfupi kwenda na kutoka Mwanza wanachohofia ni mfumo wa ukarabati wa ndege hizo unavyoendeshwa.

Januari 24 mwaka huu fly540 lilizindua rasmi safari za ndege kati ya Dar es Salaam na jiji la Mwanza ambapo itatoa huduma zake kila siku isipokuwa Jumamosi.

Mwishoni mwa Januari ndege ya kampuni ya Fly540 ilianguka ikijaribu kupaa kwa majaribio katika shamba la mahindi na mihogo lililo pembeni mwa uwanja wa ndege wa Wilson wakati ikijiandaa kuruka.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo Bwana Albanus Kioko amesema ndege hiyo namba 5X-FFD ikiwa katika njia ya kurukia ilianguka pembezoni mwa uzio wa uwanja na kutoa kelele kubwa katika eneo hilo.

“Ilianza kuondoka vizuri, lakini ilipofikia karibu na mwisho wa njia ya kurukia nilisikia muungurumo kutoka katika moja ya injini zake na baadae kuanguka katika shamba hilo la mahindi,” alisema Bwana Kioko.

Ripoti ya ajali iliyotolewa inasema ndege hiyo iliyotengenezwa kwa muundo wa kubeba mizigo imeeleza kwamba chanzo cha ajali hiyo ni moja ya injini zake kukosa nguvu wakati ikitaka kuruka ambapo ilishindwa na kuanguka.

Aidha uchunguzi wa ajali hiyo uliotolewa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya (KCAA) kushindwa huko kufanya kazi kwa moja ya injini za ndege ya kampuni ya Fly540 ndiko kulikochangia ndege hiyo kushindwa kuruka.

Watu wanne waliokuwa kwenye ndege hiyo ambao hawakujeruhiwa waliripotiwa kuchukuliwa hadi hospitali ya Nairobi kwa ajili ya matibabu ingawa imeelezwa hadi sasa hali zao zinaendelea vizuri.

Mkuu wa Polisi wa viwanja vya ndege nchini humo James Mugera alisema uchunguzi zaidi kuhusiana na ajali hiyo unaendelea na taarifa zaidi zinasema pengine ndege hiyo ilishindwa kuruka baada ya tairi la mbele la ndege hiyo kupasuka ikijiandaa kupaa.

Chanzo cha kuaminika kutoka Uwanja wa ndege wa Wilson kimesema ndege 5X-FFD licha ya kufanyiwa matengenezo haikutengemaa kwa ajili ya kuanza safari jambo lililochangia kutokea kwa ajali hiyo.

Hii ni ajali ya pili kwa ndege za kampuni ya Fly540 kutokea ikifuatiwa na ile ya ndege namba F27’s iliyotokea mwaka 2009 wakati ikitua kwenye ardhi ya Somalia kama ndege ya kukodishwa.

Ingawa mpaka sasa hakuna taarifa zozote zinazoonesha kutokea kwa ajali kwa ndege ya abiria za kampuni ya Fly540 wasiwasi unaongezeka kutokana na matukio hayo ya ajali za ndege zinazopishana kwa kipindi cha miaka miwili tu.

Katika mazungumzo yao kuhusiana na suala hilo wataalam wa mambo ya anga nchini Kenya wameshauri kitendo hicho kutojitokeza tena katika njia ya kurukia kutoka na kuingia katika kiwanja hicho cha ndege ambacho ni kikubwa na kinachozungukwa na makazi ya watu.

Kutokana na tukio hilo wataalam hao wamesema ajali za ndege za shirika hilo za mara kwa mara wanashauri kuwepo na ukaguzi wa kitaalam wa uhakika kabla ya ndege za Fly540 hazijaruhusiwa kuruka kutoka katika kiwanja hicho.

Chanzo kingine cha habari kutoka uwanjani hapo kimesema ili kulifanya eneo hilo kuwa salama kuna budi kwa kiwanja cha ndege cha Wilson kutenganishwa na majengo, makazi ya watu na majirani wanaokizunguka ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa siku za usoni ajali kama hizo itakapotokea.

Alipotafutwa Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Fly540 Bwana Dickson Ooko ili kuzungumzia suala kwa njia ya simu hakuweza kupatikana baada ya simu yake kutokuwa na majibu.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA