TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, December 21, 2010

BREAKINGNEWS............DEREVA ALIYESABABISHA KIFO CHA WAZIRI SALOME MBATIA AMEKAMATWA ..

12:34 AM


Bw.Daud Mangulla ambaye alikuwa ni dereva wa Fuso iliyogongana na gari ya marehemu naibu waziri Salome Mbatia akiwa chini ya ulinzi wa polisi
Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi (aliyekaa) akimhoji dereva huyo
Hivi ndivyo ilivyokuwa baada ya ajali iliyosababisha kifo cha marehemu Salome Mbatia



HATIMAYE baada ya kupita miaka mitatu na miezi miwili kutoka gari lenye namba za usajili T 724 AGZ Nissan Patrol alilokuwa akitumia aliyekuwa naibu waziri wanawake ,jinsia na watoto marehemu Salome Mbatia kugongwa na fuso na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wawili ,jeshi la polisi mkoani Iringa lafanikiwa kumkamata dereva wa fuso lililosababisha kifo cha naibu waziri huyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla ameueleza mtandao huu leo kuwa dereva huyo wa Fuso lenye namba T 299 AFJ ,Daud Mangulla (28) (pichani)mkazi wa mjimwema makambako wilaya ya Njombe alikamatwa jana akiwa stendi ya mabasi ya makambako .


Alisema kuwa kukamatwa kwa dereva huyo kumetokana na msaada mkubwa ulioonyeshwa na wananchi kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa jeshi hilo la polisi.

Kamanda Mangalla alisema kuwa tokea ajali hiyo itokee Octoba 24 mwaka 2007 majira yta saa 10.50 jioni eneo la Kibena barabara kuu ya Njombe -Makambako ,dereva huyo jeshi la polisi lilikuwa likiendelea kumsaka dereva huyo ambaye alitoweka baada ya ajali hiyo.

Mangalla aliwataja wengine waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na dereva wa gari ya naibu waziri huyo Anakleti Mbogela (42) na utingo wa Fuso hilo Castory Kulangwa (22) huku majeruhi walikuwa ni NIcolaus Lubava (33) na Dastan Ngonza (26).

Alisema kuwa dereva huyo alikuwa amejificha porini na baada ya kuona mambo yamekuwa kimya ndipo alipoamua kujitokeza na kuendelea na shughuli zake za kila siku eneo la mjimwema Makambako.hivyo alisema jeshi la polisi litamfikisha mahakamani dereva huyo wakati wowote kuanzia sasa.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA