TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, December 8, 2010

AJALI YAJERUHI IRINGA, BASI LA HOOD NALO LAPINDUKA INYARA MBEYA

11:44 PM


Mkazi wa kijiji cha Kigonzile Shule ya Msingi Bi Otavina Mdegela akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa wodi namba 7 akisubiri kutibiwa majeraha baada ya kugongwa na gari lenye namba T199 BEC leo eneo la Posta mjini Iringa ,Bi Otavina alikuwa amekuja mjini Iringa kumsalimia mtoto wake Tegela anayeishi Mwembetogwa mjini hapa .
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi akiwa amemkakamta dereva wa gari lilolomgonga mwanamke huyo ambalo lilikimbia na kumtelekeza barabarani kabla ya wasamaria wema kuchukua namba za gari hilo na kupiga simu polisi kwa mkuu huyu ambaye aliamua kulisaka gari hilo mwenyewe hadi anamkamata dereva huyo ambaye alikuwa amelificha gari hilo nje ya benki ya CRB Iringa
Hapa RTO Mnubi akiwa amelipata gari hilo lililosababisha ajali mtandao huu unampongeza RTO huyo kwa kazi nzuri ya kutoka ofisini na kulisaka gari hilo hadi anapolikamata.

Wakati huo huo habari zilizotua katika mtandao huu hivi punde kutoka mkoani Mbeya zinadai kuwa basi la kampuni ya Hood LTD ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda mbeya limepinduka na kujeruhi japo katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA