TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, November 7, 2010

Swahili Fashion Week kwa mwaka watatu sasa yamalizika

10:45 PM
Ally Hassan -(Daxx) the winner - Swahili Fashion Week 2010 model of the year award
Emerging designer Competition Winner Subira Wahume and Mustafa Hassanali, orgnizer of Swahili Fashion Week
Sothern Sun Best dress guest winner - Swahili Fashion Week 2010, Isabel Radick and her partner

Subira Wahure – mbunifu wa mavazavi anaechipikia Tanzania, anyaku ushindi kwanza

Ally Hassan awa mshindi kwa upande wa wanamitindo

Swahili Fashion Week kwa mwaka watatu sasa imemalizika katika viwanja vya Karimjee tarehe 6 Novemba 2010, Dar Es Salaam , Tanzania, ambapo imetoa burudani tosha katika Sanaa ya ubunifu wa mavazi, sambamba na monesho ya kibiashara

Swahili Fashion Week iliwaleta pamoja wabunifu wa mavazi 24 kutoka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili, ambapo wamekonga mioyo ya wapenzi wa Sanaa ya mavazi kwa kuonyesha ubunifu wao katika kubuni mavazi ya aina mbalimbali kwa kutumia aina mbalimbali za malighafi na mapambo.

Kwa upande mwingine Swahili Fashion Week imetoa zawadi za aina nne tofauti katika usiku wake wa mwisho, miongoni mwa zawadi hizo ni pamoja na standi bora kwa maonesho ya biashara, zawadi iliyokwenda kwa Muzu Sulemanjee wa Art & Frame.

Kwa upande wa zawadi iliyotolewa na Southern Sun Hotel imekwenda kwa Isabel Radick, baada ya kuibuka mshindi wa gauni bora, ambapo atapata fursa ya kulala hotelini hapo katika chumba cha hadhi ya juu mwishoni mwa wiki. Isabel alivaa gauni lililobuniwa na Kikoromeo mbunifu wavazi kutoka Kenya.

“Swahili Fashion Week mwaka huu pamoja na kuonesha mavazi ya wabunifu wenye majina, pia imetoa fursa kwa wabunifu wanaochipukia kuonesha mavazi lengo ni kuthamini na kukuza vipaji vyao, sambamba na kuthamini kazi kubwa zinazofanywa na wanamitindo wanochipukia.” Alisema Mustafa Hassanali, Muandaaji wa Swahili Fashion Week.

Mwaka 2009 zawadi ya mwanamitindo bora ilinyakuliwa na Victoria Martin, ambapo cheo hicho kwa mwaka huu amekabidhi kwa Ali Hassan.

Katika mchakato mzima wa wabunifu wanaochipukia, Waheru alikuwa na safari ndefu mpaka kufikia ushindi, kutoka wabunifu 31 wanaochipukia walioingia katika sindano, hatime alifanikiwa kuingi nusu fainali na kua miongoni mwa washindi walioingi fainali, ambapo wote kwa pamoja walipata fursa ya kuonesha mavazi yao na hatimae kuibuka mshindi, nafasi itkayomuwezesha kupata mfunzo ya ubunifu wa mitindo kivitendo yatakayotolewa na mbunifu wa mavazi wa siku nyingi nchini Manju Msitta. Mshind wa pili ni Zarina Suleiman na Grace Kijo amechukua nafasi ya tatu.

“ Namshukuru sana Mungu, wazazi wangu na waandaaji wa Swahili Fashion Week kwa kunifikisha hapa nilipo, Aliongea Subira Wahure kwa furaha mara tu bad ya kutangazwa mshindi.

Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery LTD, 1 & 1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.

Taarifa kwa Wahariri

Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.

Swahili fashion week in tukio ambalo linawajumuisha wabunifu wakongwe na wale wanaochipukia kuonyesha kazi zao, pia kutoa nafasi kwa wapenzi wote wa sanaa ya mavazi kujumuika pamoja na kufurahia ubunifu wa watanzania na kutoka nchi za jirani.

“Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kuwa sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa na kwa nchi za Afrika Mahariki”. Alifafanua Mustafa Muanzilishi na Muuandaaji wa Swahili Fashion Week.



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA