TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, November 19, 2010

kilimanjaro marathon yazinduliwa rasmi leo

10:59 PM

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Hermus Mwansoko (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya mbio za KILIMANJARO MARATHON ulifanyika jioni hii katika hotel ya New Afrika jijini Dar.wengine pichani ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),David Minja (pili kulia) na Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo,Leonard Tadeo pamoja na warembo walioshika tepe hiyo.
Mkurugenzi wa Wild Frentier,John Addison (kulia) akiwa katika meza moja na Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania, Suleiman Nyambui (kushoto) pamoja na Mwanariadha wa zamani,Juma Ikangaa.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa KILIMANJARO MARATHON,Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Hermus Mwansoko akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Executive Solutions,Aggrey Mariale mara baada ya kumaliza kuhutubia.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza katika uzinduzi huo.
Meneja Matukio na Miradi Maalum wa Executive Solutions,Angela Damas akitoa shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhulia katika hafla hii ya uzinduzi wa KILIMANJARO MARATHON iliofanyika jioni hii katika hoteli ya New Afika jijini Dar.
Wadau wa TBL wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.


Mbio za tisa za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Moshi tarehe 27 Februari 2011 zimezinduliwa rasmi jijini Dar es salaam leo.

Akiongea katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, wadhamini wakuu wa mbio hizo Bw. George Kavishe alisema, “sasa tumeingia mwaka wa tisa wa udhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon. Tunaona fahari kudhamini tukio kubwa zaidi la riadha hapa Tanzania ambalo limevutia ushiriki wa wadhamini mbalimbali, serikali, jamii ya Kilimanjaro na wanariadha mashuhuri kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kavishe amesema bia ya Kilimanjaro imedhamiria kuendeleza riadha nchini Tanzania kwa kupitia mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo zimeendelea kuwa kisima cha kuzalisha vipaji na kuwapa wanariadha wanaochipukia fursa ya kujipima kwa kushindana na wanariadha mashuhuri. Hili linawapa changamoto wanariadha kuboresha viwango vyao na hatimaye kupata sifa za kushiriki katika mbio kubwa zaidi za kimataifa.

Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Hermus Mwansoko amesema “Tangu Mbio hizi zilipoanzishwa mwaka 2003 zimekua chungu cha kupika vipaji katika riadha hapa Tanzania na kwakua zinaendelea kuwa kubwa zaidi kila mwaka ni matarajio yetu sote kuwa nchi yetu itaendelea kuwa na wanariadha wazuri katika mbio ndefu. Serikali inatambua mchango wa wadhamini na waandaaji wa Kilimanjaro Marathon katika kuendeleza mchezo huu na kuitangaza Tanzania maana mbio hizi huvutia sana watalii kutoka nchi mbalimbali duniani.”

Profesa Mwansoko alisema amefurahishwa na azma ya wadhamini kuendelea kudhamini Kilimanjaro Marathon na kuwapa wanariadha Watanzania fursa ya kuonyesha uwezo wao katika ushindani na wanariadha mashuhuri kutoka nchi mbalimbali.

Wadhamini wengine katika mashindano hayo ni Vodacom, Tanzania Tourist Board, Tanga Cement, DT Dobie, Tanzanite One, KK Security, Keys Hotel na Maji ya Kilimanjaro.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA