TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, June 5, 2010

Mandela kuhudhuria Kombe la Dunia

10:14 AM


Bw Nelson Mandela

Bw Nelson Mandela

Waziri wa michezo wa Afrika Kusini amesema, aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nelson Mandela atahudhuria ufunguzi wa sherehe za Kombe la Dunia.

Makhenkesi Stofile amesema Mandela mwenye sifa ya kupinga ubaguzi wa rangi aliomba tiketi kwa ajili ya siku ya ufunguzi na kufunga mashindano hayo.

Awali Mandela alisema alikuwa mdhaifu sana kuhudhuria shindano hilo linaloanza wiki ijayo.

Bw Mandela atakayefikisha umri wa miaka 92 mwezi ujao, alifanya kampeni ya kutaka Kombe la Dunia kufanyika Afrika Kusini.

Bw Stofile amesema, "Mandela ametaka kuhudhuria Kombe la Dunia."

Shirika lake la hisani, Mandela Foundation, halijathibitisha kuhudhuria kwake, wakieleza kuwa ni kutokana na sababu za kiusalama.

Takriban watu 350,000 wanatarajiwa kutembelea Afrika Kusini kwa ajili ya Kombe la Dunia, ambapo inafanyika barani Afrika kwa mara ya

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA