TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, May 26, 2010

Raisi kuzuru Kibosho na Marangu (Kilimanjaro) leo

12:07 PM
Picture
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Jakaya Kikwete,kesho anatarajia kufungua kituo cha polisi cha kata ya Ukaoni, Kibosho, wilayani Moshi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja mkoni Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa Mkoa, rais Kikwete pia atafungua tawi jipya la benki ya CRDB huko Marangu Mtoni, kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam jioni.

Taarifa hiyo pia inaonesha kuwa rais Kikwete aliewasili jioni leo akitokea Nairobi, angewakabidhi vyeti wananchi waliochangia fedha kwenye harambee ya CCM iliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema mwezi huu, na kupatikana sh. mil 200. Zoezi hilo linafanyika kweye ikulu ndogo ya rais iliyoko Moshi.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA