TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, April 6, 2010

MOVIE YA WAINGEREZA NA WATANZANIA NCHINI UINGEREZA

6:29 PM
Ni movie iliyowashirikisha baadhi ya watanzania na waingereza nchini Uingereza inayojulikana kwa jina la KINGKONG.Watanzania walioshiriki movie hii mwanzo walikuwa wanajishughulisha na sarakasi na sasa wamegeukia kwenye filamu mmoja anaitwa Hilal Majaliwa na mwenzake anajulikana kwa jina la Nasoro.Kwa dondoo nilizopewa na Hilal Majaliwa aliyenitumia picha hizi ameniambia movie hii imechukuwa takribani mwaka mmoja tangia ishutiwe na mpaka leo bado haijatoka ipo studio ikifanyiwa kazi.Malipo ambayo wamepewa ni mazuri ukilinganisha na malipo ambayo wanalipwa wasanii wa kitanzania hapa nchini,Kwakweli hata ukiangalia picha utagundua movie hii imegharimu pesa nyingi maana hata location ni za kutengeneza

Hawa nyani sio nyani wenyewe kabisa ni nyani watu ambao wametengenezwa

Angalia jinsi nyani walivyokaa tayari kwa picha

Nyani mkubwa akiwa amezungukwa na watu,Nyani kama huyu ni wa kutengeneza

Dada huyu ni mmoja wa waigizaji katika movie hii

Majaliwa akiwa na wenzake kwenye setting

Angalia hii location iliandaliwa kabisa,Ni vitu vinavyofanya filam zinakuwa za gharama kubwa maana kutengeneza location si kazi ndogo lakini tutafika tuu na sisi huko maana hata wao miaka hiyo walikuwa kama sisi

Watu wakiwa kwenye set

Kama nilivyosema filam hii ni mchanganyiko wa Waingereza na Watanzania

Nakuomba Mdau wangu Majaliwa unitumie na picha za vifaa mlivyofunga wakati mnarekodi na Production crew nzima ili wadau wengine waone production za nje zinavyokuwa

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA