TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, March 31, 2010

Kenya: Wapiganaji wa Al Shabaab hawapo

4:16 PM
Wakuu wa serikali ya Kenya wamekanusha madai kuwa nchi hiyo imekuwa, kituo muhimu cha wapiganaji na waasi kutoka Somalia.

Vyombo vya habari vimeangazia ripoti ya Umoja wa Mataifa ilioashiria kuwepo kwa wapiganaji wa Al Shabaab nchini Kenya. Ripoti hiyo pia inadai kuwa nusu ya wapiganaji wa kundi hilo ni raia wa Kenya.

Lakini katibu katika wizara ya usalama wa ndani Francis Kimemia, ameiambia BBC kuwa madai hayo ya Umoja wa Mataifa, hayana msingi wowote na kuwa hakuna mzazi yeyote mkenya anaweza kuwaruhusu watoto wake kwenda kuuawa nchini Somalia.

Kimemia pia amekanusha madai kuwa viongozi wa Al Shabaab wanaishi mjini Nairobi. Wapiganaji wa Al Shabaab wametishia mara kadhaa kuishambulia Kenya, kwa kuwa inasaidia serikali ya mpito ya nchi hiyo na hapo jana wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wa kundi hilo walishambulia wanajeshi wakiwa kwenye doria Kaskazini mwa Kenya.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA