
Serikali ya India inachunguza ripoti kuwa maharamia wa Kisomali wameteka nyara mashua kadhaa za nchi hiyo na zaidi ya mabaharia mia moja.
Jeshi la wanamaji nchini humo limesema mabaharia wa meli moja iliyoachiliwa huru na maharamia wa Kisomali wamesema meli zingine nyingi bado zinashikiliwa na maharamia hao.
Ripoti zingine zinasema maharamia hao wanazuilia mashua za uvuvi pekee huku zingine zikidai kuwa ni meli ya mizigo zilizokuwa zikielekea eneo la Ghuba.
Habari hizo zimetolewa baada ya jeshi la wanamaji nchini Ushelisheli na lile la muungano wa Ulaya linaloshika doria katika pwani ya Somalia kuwanasa maharamia katika meli moja iliyokuwa imetekwa nyara, kabla ya kuwakomboa mabaharia wake.
1 comments:
when was this?
Post a Comment