(pombe sio chai)Huku kukiwa na taarifa kuhusiana na mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bibi Teresia Mmbando kupandishwa cheo na kuwa katibu tawala ,baadhi ya watendaji wa kata katika Manispaa ya Iringa wameonyesha kumlalamikia mkurugenzi huyo kwa hatua yake ya kuwatetea baadhi ya vigogo katika maeneo mbali mbali ya mji Iringa ambayo kimsingi yalipigwa marufuku kupandwa mazao marefu kama mahindi .
uchunguzi wa mtandao huu umebaini mkurugenzi huyo ambaye alikuwa akipongezwa kwa msimamo wake wa kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo ambao walikuwa wakifanya biashara katika maeneo yasiyo ruhusiwa hivi sasa ameonekana kuanza kuwachanganya watemndaji wa kata baada ya kuwapigia simu za vitisho kuwataka kuacha kuendelea kusimamia sheria ndogo ndogo za mipango miji ikiwa ni pamoja na kuwatetea vigogo waliopanda mahindi kando kando ya nyumba zao.
katika kata ya Mtwivila zoezi la ufyekaji mahindi yaliyopandwa katika makazi ya watu limeonekana kushindikana kutokana na mkurugenzi huyo kuwaagiza watendaji na mgambo kuacha kuwaagiza wananchi kutekeleza agizo la mipango mijni kama walivyoagizwa na ofisi ya mkurugenzi huyo.
Afisa mtendaji wa kata ya Mtwivila Kunibelt Kivinge amesema kuwa msahama wa mkurugenzi huyo kwa mtumishi wa CRDB ambaye amepanda mahindi nje ya nyumba yake kinyume na utaratibu umeendelea kuleta matabaka katika kata hiyo.
Kwani anasema kuwa hatua ya kurugenzi kuwapigia simu watendaji na kuwataka kuacha kumwagiza mtumishi huyo CRD ambaye ni rafiki wa karibu na mkurugenzi huyo unachangia kuwavuruga wakazi wa kata hiyo .
Hata hivyo mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bibi Mmbando hakuweza kupatikana ili kujibu tuhuma hizo dhidi yake na jitihada za kumtafuta zinaendelea kufanywa na mtandao huu.
0 comments:
Post a Comment