Rais Barrack Obama wa Marekani amesema hana nia yoyote ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Yemen au Somalia kupambana na makundi ya wanamgambo wa kiislamu, licha ya kuongezeka kwa vitendo vya kigaidi katika mataifa hayo.Kwenye mhojiano na jarida moja nchini marekani Rais Obama amesema anaamini njia muafaka wa kutatua tatizo hilo ni kupitia ushirikiano na washirika wake wa kimataifa.
Amesema anaamini kuwa kina na ngome ya kundi la Al Qaeda ni katika maeneo ya mipaka ya Afghanistan na Pakistan.
0 comments:
Post a Comment