TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, January 27, 2010

Ndege ya Ethiopia haikufuata maelekezo

2:33 AM

Maafisa wa Lebanon wamesema, ndege ya Ethiopia iliyoanguka baharini huko Beirut siku ya Jumatatu haikuelekea upande uliopendekezwa na mnara wa kuongozea ndege.

Maafisa wa serikali wamesema rubani wa ndege ya Ethiopia alishauriwa kubadili mwelekeo, lakini akaenda upande tofauti.

Haijafahamika wazi kwanini hilo lilitokea, au kama ilikuwa nje ya uwezo wa rubani.

Serikali inaendelea kutafuta miili ya watu 90 waliokuwepo kwenye ndege hiyo, ambao wote wanasadikiwa kufariki dunia.

Watu zaidi ya 24 wameopolewa kwenye bahari ilipodondoka ndege hiyo mpaka sasa.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA