| | |
Wachezaji watano wametajwa kugombea tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anayetambuliwa na BBC mwaka 2009.
Waliotajwa ni: Didier Drogba (Chelsea na Ivory Coast), Michael Essien (Chelsea na Ghana), Samuel Eto'o (Inter Milan na Cameroon), Tresor Mputu Mabi (TP Mazembe na DR Congo) na Yaya Toure (Barcelona na Ivory Coast).
Namba ya kutuma ujumbe au SMS ni +447786 200 070 ( kwa wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, hii ni tofauti na namba ya kawaida).
Unaweza kumpigia kura mchezaji wa chaguo lako mpaka tarehe 4 Januari na mshindi atatangazwa siku nne baadaye, Januari 8 huko Angola wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.
Tuzo hiyo ya hadhi kubwa ndiyo pekee ya aina yake kutolewa kutokana na idadi ya kura zinazopigwa na mashabiki wa soka.
Mshindi wa mwaka jana alikuwa Mohamed Aboutrika wa Al Ahly na Misri, aliyeisadia nchi yake kutetea kikombe cha kombe la mataifa ya Afrika na kuiwezesha timu yake kuchukua kombe la ligi ya vilabu bingwa Afrika.
Waliowahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika
2008 - Mohamed Aboutrika
2007 - Emmanuel Adebayor
2006 - Michael Essien
2005 - Mohamed Barakat
2004 - Jay-Jay Okocha
2003 - Jay-Jay Okocha
2002 - El Hadji Diouf
2001 - Sammy Kuffour
2000 - Patrick Mboma
0 comments:
Post a Comment